Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jenerali Mkunda avisha Nishani Kanda ya Mbeya

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Maafisa na Askari wa JWTZ jijini Mbeya leo tarehe 26 Machi 2025. Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyotambua mchango wao katika kulitumikia taifa kwenye nyanja ya Ulinzi. Aidha,amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakuwa salama wakati wote. Nishani hizo ni Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema,Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ na Nishani ya Jumuiya ya SADC.

Dcea yamnasa Kinara wa Mirungi , Yatekeza Ekari 285.5 Same

  Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya msako maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, inawashilia watu Saba akiwamo kinara wa biashara ya mirungi na kufanikiwa kuteketeza Ekari 285.5 za mashamba ya aina hiyo ya dawa za kulevya. Msako huo ulioanza Machi 19 Hadi 25,mwaka huu ulifanikisha kumkamata kinara wa biashara hiyo Interindwa Zinywangwa Kirumbi maarufu kama mama Dangote aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu. Akizungumza baada ya kukamilisha msako huo, Kamishna Jenerali wa DCEA,  Aretas Lyimo, amesema kwamba  mama Dangote ni, mzalishaji na msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi nchini.  Kwa zaidi ya miaka 30, anaendesha mitandao ya biashara haramu ya mirungi na kusimamia masoko ya dawa hizo za kulevya mahali tofauti nchini,  huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria. "Mwaka juzi Mamlaka ilifanya msako katika Wilaya hii, tulitoa elimu kw...

Rais Mstaafu Kikwete Awasilisha Ujumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Samia Kwa Rais wa Algeria, Tebboune

Algiers, Machi 26, 2025 – Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa Mhe. Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria. Katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili walijadili kwa kina kuhusu uhusiano wa muda mrefu na wa kindugu kati ya Tanzania na Algeria, wakisisitiza mshikamano na ushirikiano imara ulioanzia enzi za harakati za ukombozi wa Afrika, na waasisi wa mataifa hayo mawili. Pia walijadili njia za kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano katika sekta kama biashara, uwekezaji, elimu, afya na ulinzi. Mhe. Kikwete aliwasilisha dhamira ya Mhe. Rais Samia ya kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa haya mawili, akibainisha maono ya pamoja ya ukuaji wa uchumi na utulivu wa kikanda. Kwa upande wake, Rais Tebboune alieleza kuwa anathamini sana urafiki wa Tanzania na akaeleza utayari wa Algeria wa kuendeleza ushirikiano ka...

Waziri Mkuu Aagiza Kituo cha Afya Mama Ngoma Kupandishwa Hadhi

- Asema muwekezaji amefanya kazi kubwa lazima Serikali imuunge mkono. - Awagiza watendaji wa Halmashauri kusimamia ukamilishaji wa miradi. WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, amemuagiza Waziri wa Afya, Jenista Mhagama na watendaji wa Wizara hiyo kukutana na kufanya mapitio ya vigezo ili kukipandisha hadhi kituo cha Afya cha Mama Ngoma kilichopo kata ya Kwakoa Wilaya ya Mwanga Mkoani kilimanjaro kuwa hospitali. Amesema mwekezaji huyo amefanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Shilingi Bilioni tano kwa kujenga majengo yenye hadhi na kuweka vifaa vya kisasa hivyo ni lazima Serikali imuunge mkono kwa kukipandisha kituo hicho. "Maliza hatua iliyobaki ipewe hadhi ya hospitali kama kuna eneo mnadhani linatakiwa kufanyiwa marekebisho mshirikiane nae, kazi anayofanya huyu ni kubwa ya kuiunga mkono Serikali ya kuwahudumia Watanzania tunamuachaje?". Alihoji Ametoa maelekezo hayo (jana Jumanne Machi 25, 2023) alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kuzindua Kituo Cha Afya cha Mama Ngoma kilichop...

Mbunge Muhongo Achangia Mifuko 250 ya Saruji Kwenye Harambee Sekondari ya Nyabakangara

  Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amechangia mifuko 250 ya saruji kwenye ujenzi wa shule ya sekondari Nyabakangara. Harambee hiyo iliyofanyika machi 25,2025 kwenye Kitongoji cha  cha Kamatondo Kata ya Nyambono ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo wa CCM,wazawa wa Kata hiyo na wadau wa maendeleo wakiwemo wa elimu. Akizungumza kwenye harambee hiyo mbunge Muhongo amesema elimu bado ni kipaumbele ndani ya jimbo na ndiyo inayopelekea jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule. Amesema ili kumsaidia mwananchi wa Musoma Vijijini ni pamoja na kumpa elimu mtoto wake kwa manufaa ya baadae. Mbunge Muhongo amesema kila mmoja anakaribishwa kwenye jimbo la Musoma vijijini kuchangia maendeleo ya elimu ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa. "Ndugu zangu kipaumbele chetu namba moja bado ni elimu na ndio maana tunafanya jitihada mbalimbali zikiwa ni pamoja na kuendesha harambee za ujenzi wa shule na kuandaa mi...

Waziri Wa Mambo ya Nje wa Drc Awasili Nchini

Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi ambaye pia ni  Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Mhe. Therese Kayikwamba Wagner amewasili nchini. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Mhe. Wagner amelakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo. Akiwa nchini Mhe. Wagner anatarajia kuwasilisha ujumbe maalum wa Mheshimiwa Rais Tshisekedi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.