Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jela Miaka 30 Kwa Kubaka Mjukuu Wake

Na Dawati la Habari Polisi ;Mwanza Mahakama ya Wilaya Sengerema, mkoani Mwanza, imemuhukumu Lucas Maselele (56), mkazi wa kijiji cha Lugata wilayani humo kwenda jela miaka 30   baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka  mjukuu wake (13) (jina linahifadhiwa) kwa sababu za kisheria. Hukumu hiyo imesomwa  leo Machi 13,2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka Katika kesi hiyo ya Jinai namba 16492/2024 . Awali, Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Nyamhanga Tissoro aliieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 04, 2024, katika Kijiji cha Lugata, wilaya ya Sengerema kwa kumbaka mjukuu wake wakati mke wake ameenda msibani mpaka alipofumaniwa na mke wake akifanya kitendo hicho kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(e) pamoja na kifungu cha 131(1) vya sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya Kwanza tarehe 14.06.2024 baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi na kusomewa shta...

Kamati ya Kudumu ya Bunge Yaridhishwa na Utekelezaji Mradi wa Umwagiliaji Nyida, Shinyanga

Ni mradi wa Umwagiliaji unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya  Umwagiliaji (NIRC)  NIRC ;Shinyanga.  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,Kilimo na Mifugo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi inayofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), ikiwemo ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Nyida mkoani Shinyanga. Kamati hiyo imesema kinachofanywa na Tume hiyo kinaendana na thamani ya fedha inayowekezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miradi ya umwagiliaji nchini. Akizungumza katika ziara fupi ya kukagua miradi hiyo mkoani Shinyanga, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deodatus Mwanyoka, amesema kamati inaridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba thamani ya fedha inaonekana.  “Hata kwa macho ukiangalia ujenzi wa ofisi, bwawa na miundombinu mingine inaridhisha na Sh8 bilioni  zilizoanza kufanyiwa uwekezaji zinaoneka." Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa anaamini malipo yaliyobaki kiasi cha Sh5. 6 bilioni ili kukamilisha mradi huo unaotarajia kugharimu  Sh13. 6 ...

Kamati ya Kudumu ya Bunge Afya na Masuala ya Ukimwi yaipongeza Serikali ya Mkoa wa Mara

  Na Shomari Binda-Musoma  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi imeipongeza serikali ya mkoa wa Mara kwa usimamizi wa fedha za ujenzi zinazoletwa na serikali kuu kwenye hospital ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Pongezi hizo zimetolewa leo machi 13,2025 na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hassan Selemani Mtenga baada ya kutembelea mkoa wa Mara na kufika kwenye hospitali hiyo. Amesema serikali ya mkoa chini ya mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi imekuwa na usimamizi mzuri wa wakandarasi na fedha zinazoletwa na serikali kuona hospitali hiyo inakamilika na kutoa huduma ipasavyo. Mtenga amesema Kamati imeridhidhwa na ujenzi wa ukamilishwaji wa hospitali hiyo iliyoanza kujengwa toka mwaka 1976 na serikali ya awamu ya kwanza. Amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeleta fedha shilingi bilioni 4 za ukamilishaji na maendeleo ni mazuri ikiwemo usimamizi wa fedha. " Tunaipongeza serikali ya mk...

Waziri Mkuu Amesema Serikali itaendelea Kuboresha Mazingira ya Ujasiriamali

_▪️Amesema lengo ni kuongeza kipato cha wananchi kwa kujikita kwenye ufundi mahiri._ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea na mkakati wa kufungua milango ya ujasiriamali kwa kutekeleza sera na programu mbalimbali zitakazowasaidia wananchi kuendana na soko la ajira ili kujiongezea kipato. Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi Machi 13, 2025) alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Amali ya Makomelo iliyopo Nzega mkoani Tabora ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 1.6 . Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali iliamua kutenga kiasi cha shilingi bilioni 44.7 kwa ajili ya ujenzi shule za amali katika kila mkoa ili kuwawezesha Watanzania kupata elimu ya mafunzo maalum yatayowasaidia kujiajiri au kuajiri wengine na hatimaye kujikwamua kiuchumi. “Lengo letu ni kupanua na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia sambamba na kutoa elimu yenye ujuzi na vitendo vyenye kukidhi katika ulimwengu wa ajira.” “Malengo ya Serikali ni kuwafikisha vijana kupata ujuzi ...

Majaliwa Azindua Kituo cha Mabasi Nzega Mjini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 13, 2025 amezindua kituo kipya cha Mabasi cha Nzega mjini,katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.327. Akizungumza baada ya kuzindua kituo hicho ambacho utekelezaji wake umefikia asilimia 100, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza halmashauri hiyo kwa uamuzi wa ujenzi wa kituo hicho kwani kitaibua fursa za biashara kwa wakazi wa eneo hilo. “Kituo hiki ni kizuri na kimejengwa kwa ubora, kituo hiki kinatakiwa kianze kutumika ili wananchi waanze kunufaika nacho, Watumishi wa halmashauri ongozeni Wana-Nzega kunufaika na fursa katika eneo lenu” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa halmashauri hiyo kuongeza vibanda vya wafanyabiashara badala ya vichache ambavyo vimejengwa mpaka sasa. “Tunataka wananchi wengi zaidi wanufaike, ongezeni vibanda, huu ni ubunifu mzuri sana utasababisha wengi wanufaike, waleteni wajasiriamali hapa wapate rizki zao, mkifanya hivyo mtaongeza mzunguko wa fedha” Kadhalika, Mheshimiwa...