Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kiwanda kikubwa cha sukari ya viwandani kujengwa Tanga-Dkt Samia

Na MASHAKA MHANDO, Pangani.  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itajenga Kiwanda Kikubwa cha Sukari ya viwandani eneo la Bandarini Jijini Tanga ili kujitosheleza na mahitaji hapa nchini na kupunguza matumizi ya Dola. Aliyasema hayo jana mjini Pangani wakati wa ziara yake ya Wilayani Pangani baada ya kuweka jiwe la Msingi Kwenye barabara ya Tanga-Pangani pamoja na daraja la Mto Pangani ambalo litakuwa mkombozi Mkubwa Kwa wananchi. Alisema malighafi ya kiwanda hicho itatokea wilaya ya Pangani kutokana na kwamba wilaya hiyo inakwenda kubadilika kutokana na kuja na kilimo kikubwa cha Miwa ndani ya wilaya hiyo. "Pangani inabadilika na itaendelea kubadilika kwa sababu tunakwenda kuja na kilimo kikubwa cha miwa shamba likalokuwa pembeni ya mto Pangani na  Kiwanda kikubwa cha sukari ya viwandani kujengwa Tanga-Dkt Samia*  cha sukari kitajengwa Tanga Jiji"Alisema Rais Dkt Samia " Tuna Viwanda vingi vya sukari lakini sukari ya viwanda...

Mnadhimu Mkuu Wa Jwtz Amesema Jumuiya Ya Afrika Mashariki Inaweza Kujitegemea Kiviwanda

 MNADHIMU mkuu Wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman amewataka wakuu wa mashirika na viwanda vya majeshi katika nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutumia utafiti,Sayansi na Teknolijia katika uzalishaji wa bidhaa ili kuhakikisha mashirika na viwanda hivyo vinazalisha bidhaa zenye kukidhi mahitaji ya soko ndani na nje ya  ukanda huo. Akizungumza wakati akifunga mkutano wa siku mbili ambao umewahusisha wakuu wa mashirika na watendaji wa viwanda vya majeshi kutoka nchi nane za jumuiya ya afrika mashariki jijini Dar es Salaam,Luteni Jenerali Othman amesema Maendeleo yoyote ya viwanda yanayodumu kamwe hayawezi kutenganishwa na uwekezaji katika sayansi na teknolojia, pamoja na utafiti na maendeleo. Kwa sababu hiyo, amewataka wakuu hao wa mashirika na viwanda vya majeshi katika jumuiya hiyo kuhakikisha wanalizingatia jambo hilo katika kila hatua wanayochukua na kwamba Kwa kufanya hivyo wataweza kuhakikisha kuwa viwanda vya maj...