📌 Dkt. Samia achagiza mapinduzi ya nishati Afrika 📌 Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia yajadiliwa kimataifa Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani kuwekeza katika sekta ya nishati nchini. Akizungumza leo Februari 12, 2025 jijini New Delhi, India katika Mkutano wa Mawaziri wa Nishati kutoka India, Sudan, Malawi, Rwanda, Nepal, Brazili pamoja na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali kutoka India Dkt. Biteko amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha Nishati Safi ya Kupikia inapatikana kwa urahisi na gharama nafuu. Mwaka 2022 Serikali ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilisisitiza matumizi ya nishati safi na kueleza athari za matumizi ya nishati isiyokuwa safi kwa kuanzisha mjadala wa kwanza kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na faida zake kiuchimi na Kijamii. Dkt. Biteko ...
Marato tv - Sauti ya Jamii