Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Anadi Fursa Za Uwekezaji Sekta ya Nishati Kimataifa

📌 Dkt. Samia achagiza mapinduzi ya nishati Afrika 📌 Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia yajadiliwa kimataifa Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani kuwekeza katika sekta ya nishati nchini. Akizungumza leo Februari 12, 2025  jijini New Delhi, India katika Mkutano wa Mawaziri wa Nishati kutoka India, Sudan, Malawi, Rwanda, Nepal, Brazili pamoja na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali kutoka India Dkt. Biteko amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha  Nishati Safi ya Kupikia inapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.  Mwaka 2022 Serikali ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilisisitiza matumizi ya nishati safi na kueleza athari za matumizi ya nishati isiyokuwa safi kwa kuanzisha mjadala wa kwanza kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na faida zake kiuchimi na Kijamii. Dkt. Biteko  ...

Bilioni 30 za Mradi wa Maji Taka Kuuweka Mji Wa Musoma Katika Hali ya Usafi

Na Shomari Binda-Musoma  SHILINGI bilioni 30 zinazo tekeleza mradi wa maji taka manispaa ya Musoma zinatarajia kuuweka huo katika hali ya usafi. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka alipotembelea eneo la mradi kukagua chughuli zinazo fanyika. Amesema kukamilika kwa mradi huo kutawanya wananchi wa manispaa ya Musoma kuunganishwa na mradi huo kuelekeza maji taka wanayo zalisha. Chikoka amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na shirika la maendeleo la Ufaransa kwa mradi huo kwaajili ya kuweka mji wa Musoma kwenye hali ya usafi. Mkuu huyo wa Wilaya amesema kupitia mradi huo  vyoo zaidi ya 370 vimejengwa kwenye shule na maeneo ya mikusanyiko ya watu kwaajili ya kutoa huduma. " Tunamshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwaajili ya mradi huu ambao sasa unakwenda kuweka mji wetu safi kutokana na maji taka yanayozalishwa. " Kupitia mradi huu wananchi wataunganishwa kwenye mfumo na kuhakikisha maji taka yote yanayo zalishwa yanaelekezwa eneo la mradi...

Wenye Matatizo ya Macho Waendelea Kupatiwa Huduma Za Kibingwa Hospitali ya Mwalimu Nyerere

Na Shomari Binda-Musoma  WANANCHI wenye matatizo ya macho mkoani Mara wameendelea kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa kwenye hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Huduma hizo wanazipata kutoka kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya rufaa ya kanda Bugando kwa kushirikiana na madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo. Akizungumza hospitali hapo mganga mfawidhi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk.Osmundi Dyegura amesema wananchi wameendelea kupokelewa na kupata huduma zikiwemo za oparesheni. Amesema madaktari hao wameendelea kuwaona wananchi na kuwafanyia uchunguzi na wanaobainika kufanyiwa oparesheni wanapewa huduma hiyo. Dk.Dyegura amesema hospitali imekuwa na utaratibu wa kuwaleta madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kila mwezi na safari hii wanao wa magonjwa ya macho na kuwaomba wananchi kuwatumia kupata huduma. Amesema huduma zimeanza februari 10 na zinaendelea kutolewa hadi ijumaa ya februari 14 na kudai hiyo ni fursa ya wananchi kutotumia gharama ku...

India Kuwekeza Katika Sekta ya Nishati Nchini

📌 *Ni kupitia mazungumzo kati ya Dkt. Biteko na Waziri wa Petroli na Gesi Asilia India* 📌 *Gesi, Nishati Safi ya Kupikia na Bayofueli zatajwa*  ðŸ“Œ *India yaipongeza Tanzania usambazaji umeme vijijini* 📌 *Dkt. Biteko akaribisha wawekezaji,wafanyabiashara kutoka India* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Petroli na Gesi Asilia wa India, Mhe. Hardeep Singh kuhusu nia ya nchi hiyo kuzidi kuimarisha biashara kati yake na Tanzania kupitia sekta binafsi, kufanya uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati na kujengea uwezo wataalam. Mazungumzo hayo yamefanyika Februari 11, 2025  jijini New Delhi nchini India katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Nishati nchini humo. Dkt. Doto Biteko amemweleza Waziri Singh kuwa milango ya uwekezaji Tanzania ipo wazi  na kampuni mbalimbali kutoka India zinaweza kuwekeza kwenye  maeneo mbalimbali ikiwemo ya umeme, usambazaji wa gesi ya mitungi (LPG) na uagizaji wa mafuta kw...

Mchimbaji mdogo wa dhahabu ampa Tano Rais Dkt. Samia

 *Vijana watakiwa kuwa waaminifu* SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanapata mitaji, leseni na matumizi ya teknolojia katika shughuli za uchimbaji wa madini na kuwezesha  kuchimba kisasa. Akizungumza katika mahojiano maalum mmiliki wa Mgodi wa Kwasakwasa uliopo kijiji cha Msesule kata ya Mapogoro, wilayani Mbarali mkoani Mbeya, mwanadada Amagite Mkumbwike amesema, Serikali ya Awamu ya Sita  imeweka mazingira wezeshi ikiwemo bei nzuri sokoni ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika zaidi. “Nikiwa mchimbaji mdogo na mmiliki wa mgodi wa Kwasakwasa, nitaendelea  kumuunga mkono Rais Samia kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana na kurudisha faida kwa kile kinachopatikana katika vijiji vinavyozunguka mgodi wetu,”amesema na kuongeza, “Serikali imerahisisha vitu vingi ikiwemo kuhakikisha bei ya dhahabu sokoni zinakuwa juu ili wachimbaji wadogo tunufaike. Tumee...

Tanzania Yahakikisha Usalama Wa Chakula Comoro

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa  vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu,februari 11 Mwaka huu amekutana na kufanya Mazungumzo na Ujumbe maalumu kutoka Serikali ya Comoro unaoshughulikia azma ya nchi hiyo kuimarisha biashara ya bidhaa za chakula.  Ujumbe huo uliongozwa na Bw. Snehal SONEJI, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa nchini Comoro.  Washiriki wengine kwenye Mazungumzo hayo ni Dkt. Hamza A. Azali, Mamlaka ya Utafiti wa Kilimo, Mazingira na Uvuvi (INRAPE), na Bw. Abdillahi M'Saidie, Rais wa Jumuiya ya Wafugaji, Wakulima, Wavuvi na Sanaa nchini Comoro. Ujumbe kutoka Serikali ya Comoro ulijulisha kuwa ulitembelea Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Februari, 2025 ambapo walibahatika kukutana na kufanya mazungumzo na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kukutana na Ushirika wa Uzalishaji katika Chuo cha Kilimo cha SOKOINE, pamoja na kutembelea miradi ya kilimo.  Kufuatia mazungumzo yao, Taasisi za Tanzania zimeon...