Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wassira Atembelea Kaburi La Baba Wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Butiama Kijijini Butiama

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Stephen Wassira ametembelea kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Butiama, leo Februari 3, 2025 akiwa ziarani mkoani Mara ambapo pia amezungumza na wazee wa Butiama.

Mgombea Wa Urais Wa Ccm Dkt Samia Suluhu Hassan Kutambulishwa Kwa wanachama Feb 5- 2025 Jijini Dodoma

 

Mbunge Ndejembi Amkosha Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko Kwa Maendeleo Chamwino

 📍Chamwino ▪️RAIS SAMIA AMEING'ARISHA CHAMWINO KIMAENDELEO - DKT. BITEKO ▪️Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 13 elimu ya Sekondari Chamwino ▪️Uboreshaji wa miundombinu shilingi bilioni 17.9 zimetumika ▪️Vijiji  vyote 47 Chamwino vimewashwa umeme Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuing'arisha Chamwino kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo hilo. Hayo yamebainishwa leo Februari 02, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka 5, (2020  2025) iliyowasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi.  "Nimemsikiliza Mhe. Ndejembi akieleza kazi kubwa ambayo Serikali imeifanya hapa Chamwino, ni dhahiri kwamba Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Dkt. Samia imefanya kaz...

Rc Mtambi asisitiza usuruhishi wa migogoro na elimu ya kisheria kwa wananchi.

  Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesisitiza elimu ya kisheria na usuruhishi ipewe kipaumbele na kutolewa kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake leo Februari 3 na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki na siku ya Sheria nchini. Akitoa salam za serikali amesema elimu ni suala la muhimu wananchj kuipata ili kuweza kuwa na ufahamu wa kisheria na kuepukana na migogoro mbalimbali. Amesema wananchi wakiwa na elimu itakuwa rahisi kukaa katika meza ya usuruhishi na kufikia makubaliano bila kuingia kwenye Mahakama. RC Mtambi amesema serikali inaendelea kutatua migogoro ili kuipunguzia mashauri Mahakama na kuendelea kuwa na ufanisi kwenye utendaji. " Mimi kama mkuu wa Wilaya kwenye ofisi yangu nimetenga siku ya kuwasikiliza wananchi na yanapokuja masuala ya kisheria tunashirikiana na wadau kuyasikiliza. " Serikali ipo tayari kushirikiana na Mahakama hususani katika eneo la usuruhishi wa migogoro inapotuf...

Rais Samia Awahutubia Watanzania Kupitia Majaji Siku ya Sheria Nchini Jijini Dodoma

 Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.  Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja wa Mahakama Kuu wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 03 Februari, 2025. Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 03 Februari, 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia, Majaji, wageni waalikwa pamoja na wananchi kwa ujumla kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 03 Februari, 2025.