📍Chamwino ▪️RAIS SAMIA AMEING'ARISHA CHAMWINO KIMAENDELEO - DKT. BITEKO ▪️Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 13 elimu ya Sekondari Chamwino ▪️Uboreshaji wa miundombinu shilingi bilioni 17.9 zimetumika ▪️Vijiji vyote 47 Chamwino vimewashwa umeme Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuing'arisha Chamwino kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo hilo. Hayo yamebainishwa leo Februari 02, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka 5, (2020 2025) iliyowasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi. "Nimemsikiliza Mhe. Ndejembi akieleza kazi kubwa ambayo Serikali imeifanya hapa Chamwino, ni dhahiri kwamba Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Dkt. Samia imefanya kaz...