Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu amwakilisha Mhe. Rais Dkt Samia Katika Sherehe Za Uapisho wa Rais wa Msumbiji

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 15, 2025 ameshiriki sherehe za uapisho wa Rais wa Msumbiji akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.  Katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Maputo,  ambapo baada ya kiapo hicho  Rais Daniel Chapo ametaja vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa, kuimarisha usalama, kuboresha SEKTA za elimu, afya na kilimo.  Mbali na hayo RAIS, pia Rais Chapo amewaomba wana Msumbiji wafanye kazi kwa ushirikiano pia ameahidi kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali kwa kupunguza  ukubwa wa Baraza la Mawaziri. Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane kutoka chama cha Podemos aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika  Oktoba 9, 2024.  Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawa...

Majaliwa akutana na Rais wa Msumbiji Daniel Chapo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Msumbiji Daniel Chapo kwenye makazi ya Rais, Ponta Vermelha, Maputo nchini Msumbiji. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za uapisho zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Maputo Januari 15, 2025.

Rais Samia Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu Jan 17 Dodoma

 

Rais Samia akutana na Mabalozi sherehe mwaka mpya Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.

WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika kesho Januari 15, 2025.  Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9, 2024.  Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake. Sherehe za uapisho zitafanyika katika uwanja wa Independence (Uhuru) jijini Maputo.

Michuano ya CHAN yaahirishwa,Sasa Kufanyika August 2024

Kwa Mujibu Taarifa iliyotolewa na CAF, Miongoni mwa sababu zilizochangia kusogezwa mbele kwa Michuano ya CHAN ni pamoja na kutokamilika kwa miundombinu ya kusakatia Kabumbu ikiwemo Viwanja pamoja na hoteli katika Mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania kulikotarajiwa kufanyika Michuano hiyo.  Kusogezwa mbele kwa Michuano ya CHAN hadi mwezi August kunalenga kuyapata fursa Mataifa hayo kukamilisha maandalizi yanayohitajika ili kuwezesha Michuano kufanyika kwa ufanisi.  Hata hivyo CAF imesema Droo kwa ajili ya kupanga Makundi ya CHAN itafanyika Januari 15 Mwaka huu Jijini Nairobi Nchini Kenya kama ilivyokuwa imepangwa