Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Samia ameiheshimisha Tanzania Matumizi ya Nishati safi-Majaliwa

  _Asema Watanzania tunapaswa kumuunga mkono_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiheshimisha Tanzania katika hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kutokana na umuhimu wake kwenye afya ya binadamu na utunzaji wa mazingira. Amesema kuwa kutokana na jitihada hizo, mashirika ya kimataifa yameonesha nia ya kumuunga mkono ikiwemo kufanya mkutano mkubwa wa nishati safi Afrika hapa nchini. “Watanzania tumuunge mkono Rais Dkt. Samia katika kampeni hii na kuhakikisha tunaongoza kwenye matumizi ya nishati safi barani Afrika” Amesema hayo leo (Jumanne, Desemba 31, 2024) wakati wa Tamasha la Azimio la Kizimkazi ambalo lilienda sambamba na ugawaji wa majiko 1000 ya gesi kupitia kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia. Tukio hilo limefanyika katika eneo la Kilimahewa Majumbakumi, Ruangwa mkoani Lindi. “Tunapaswa kumuunga mkono kwasababu agenda imeanzishwa na Rais wetu, dunia lazima iitambue Tanzania kama ambavyo imetambua na kuleta mku...

Wananchi wa Ngombo Waendelea Kulipwa Fidia

Na Beatus Maganja, Malinyi. Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema zoezi la kuwalipa fidia wananchi wa Kijiji cha Ngombo kilichopo ndani ya Pori la Akiba Kilombero Mkoani Morogoro linaendelea vizuri ambapo asilimia 93 ya wananchi wote tayari wamekwishalipwa fidia zao kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi katika Hifadhi hiyo na asilimia 7 ya wananchi waliosalia wanaendelea kushughulikiwa ili kukamilisha malipo yao. Akizungumzia zoezi hilo Desemba 31, 2024 wilayani humo Mhe. Sebastian amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi billioni 6.9 kulipa wananchi 1,056  ili waweze kuhama kwa hiari kutoka maeneo ya Hifadhi huku akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji 32 wilayani Malinyi kuwapokea ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku. "Kwanza si kweli kwamba wananchi wa Ngombo hatujawaambia mahali pakwenda. Katika barua yangu ya tarehe 4 Disemba, 2024  niliyowaandikia watendaji wa vijiji 32 vilivyo ndani ya wilaya ya Malinyi, nilitoa maelekezo ya kuwapok...

Waziri Mavunde asimamisha Uchimbaji Madini kwenye Mto Zila kijiji cha Ifumbo wilayani Chunya-Mbeya

▪️Aelekeza shughuli za uchimbaji madini kusimama kipindi hichi cha Masika kama ilivyoelekezwa na NEMC ▪️ Timu ya Wataalam kufanya tathmini kwa kina na kutoa taarifa ya athari ya Mazingira ▪️Akemea wananchi kuharibu mali za mwekezaji ▪️Asisitiza Sheria na kanuni kufuatwa 📍Chunya,Mbeya Waziri wa Madini, *Mh.Anthony Mavunde (Mb)* amesimamisha shughuli za uchimbaji zilizokuwa zikifanywa na kampuni ya G & I Tech Mining Company Ltd kwa kipindi hichi cha masika na pia mpaka pale tathmini ya kitaalam ya mazingira itapokamilika juu ya shughuli za uchimbaji madini kwenye Mto Zila. Ameyasema hayo Jana tarehe 30 Desemba, 2024 katika kijiji cha Ifumbo, Wilayani Chunya alipotembelea eneo la leseni ya mwekezaji ambalo lilivamiwa na wananchi na kusababisha mgogoro mkubwa na uharibifu wa mali za mwekezaji huyo. "Tumetembelea maeneo yote mawili, na sote tumejionea hali halisi ya mazingira. Ni dhamira na maelekezo ya *Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan* kuona shughuli zote za kiuchumi hususan za madi...

Tra yamkosha Askofu Mkuu Ruwa'ichi,atoa ahadi ya Ushirikiano

Askofu Mkuu Mwandamizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddeus Ruwa'ichi amesema Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam litaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhamasisha watu walipe Kodi kwa kutokana na Kodi kuwa ni suala nyeti kwa maendeleo ya Nchi. Akizungumza na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kuwashukuru Walipakodi, Askofu Mkuu Ruwa'ichi amesema Suala la kulipa Kodi na kukusanya Kodi ni suala linalohusu maendeleo ya nchi na ni sehemu ya wajibu wa Kiraia. Askofu Mkuu Ruwa'ichi ameeleza kufurahishwa na mfumo wa ukusanyaji wa Kodi unaofanywa katika kipindi cha sasa na ukaribu uliopo baina ya Mamlaka hiyo na Wananchi. "Kwa niaba ya Watanzania wenzangu niwapongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya na kuwahakikishie kwamba kadiri ya nafasi na uwezo wetu tutajitahidi kuwahimiza watu wazingatie na waenzi wajibu wa kulipa Kodi kwaajili ya Maendeleo ...

Mbunge Mathayo ampa tano Rais Samia kwa kutoa Bilioni Moja Sekta Ya Uvuvi

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshawafikia wananchi wa Musoma na kuwawezesha kiuchumi. Kauli hiyo ameitoa leo disemba 30 aliposhiriki na kuzungumza kwenye kongamano la jukwaa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Wilaya ya Musoma lililofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo. Jukwaa hilo ni muendelezo wa matukio ya Mama Samia Musoma Festival ilyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Musoma. Mathayo amesema kupitia sekta ya uvuvi pekee Rais Samia kwa manispaa ya Musoma ametoa vizimba na chakula cha samaki ikigharimu zaidi ya bilioni 1. Amesema licha ya eneo hilo la uvuvi tayari halmashauri ya manispaa ya Musoma imeanza kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake,vijana na wenye ulemavu. Mbunge guyo amesema hizo zote ni fursa za kuwawezesha wananchi kiuchumi ambazo wanapaswa kuzitumia na kujiinua. Amesema wananchi wanapaswa kuacha uvivu na kujituma kufanya kazi ili fursa zilizotolewa ziweze kuwainua. ...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amlilia Jaji Werema