Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Zahanati Mpya Yafunguliwa Kijiji cha Nyabaengere Kuongeza Utoaji Huduma za afya Vijijini

Na Shomari Binda-Musoma ZAHANATI mpya imefunguliwa leo disemba 5 kwenye Kijiji cha Nyabaengere Kata ya Musanja Jimbo la Musoma vijijini ili kuendelea kuwafikia karibu wananchi na kutoa huduma. Ujenzi wa zahanati hiyo ulianzishwa kupitia harambee iliyoanzishwa na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo huku wananchi wakichangia nguvu kazi na fedha. Kata ya Musanja yenye vijiji vitatu vya Mabuimerafuru, Musanja na Nyabaengere haikuwa na zahanati hata moja huku wananchi wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya kwenye Kata jirani ya Murangi Vijiji viwili vya Nyabaengere na Mabuimerafuru vinajenga zahanati za vijiji vyao na leo Kijiji cha Nyabaengere kimezindua utoaji na huduma za afya kwenye zahanati yake mpya. Wakizungumza kijijini hapo wananchi wameshukuru juhudi za mbunge wao kwa kuanza na harambee hadi kufikia malengo. Mmoja wa wananchi wa Kijiji hicho Malima Mugeta amesema bila jitihada na uhamasishaji uliokuwa ukifanywa na mbunge Muhongo wasinge fanikiwa....

Dkt.Biteko na Dkt.Jakaya Kikwete washiriki UDSM Marathon

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishiriki UDS Marathon iliyoandaliwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya Wanafunzi chuoni hapo. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Jakaya Kikwete, Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, Jijini Dar es Salaam.

Shirika la ActionAid Latoa Elimu kwa Wananchi Kukabiliana na Athari za Mabadiriko ya Tabia nchi na Ukatili-Dodoma

  Na Mwandishi Wetu Dodoma SHIRIKA lisilo la Kiserikali  la Actionaid Tanzania kupitia  Mradi wa TIF (Transformative Impact Fund) katika kuelekea maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia limeendesha kampeni   yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii kuendeleza kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabia nchi (Kilimo ikolojia) kwa wakulima wadogowadogo hasahasa wanawake na vijana. Akizungumza na Wananchi  mbalimbali Disemba 6,2024 wakati wa  kampeni hiyo   Katika  Kijiji cha Mloda kata ya Mlowa Barabarani wilaya ya Chamwino Mwenyekiti wa Kijiji hicho Adam Philimon amewataka jamii kuachana na mila potofu yakuwa mtoto wakike hana haki ya kumiliki adhi kama mtoto wa kiume. ''Naupimaji huu maana yake ni utambuzi kwamba je tuangalie kuna ukatili kwa sababu hii  hii ardhi siyo lazima umiliki we mwanaume,  hii ardhi  hakuna mtoto wa kike wa kunyimwa  wote wanahaki   hichi ndicho kilichokuwa kinafanyika ,'' ...

Watumishi wa Umma Katika Madawati ya Mrejesho Watakiwa Kutoa Huduma Kwa Ufanisi

 Na Hamida Ramadhan, Dodoma MWAKILISHI wa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Leila Mavika amewataka Waratibu wa Kushughulikia Mrejesho wakayatumie mafunzo waliyoyapata kuleta mapinduzi  katika  Madawati au Ofisi za Mrejesho zilizopo katika Taasisi zao  ili kufanikisha ushughulikiaji mrejesho kwa ufanisi na kwa wakati katika Ofisi za Umma kwa vile  wameaminiwa kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi. Amewataka wakawe waaminifu na wenye haiba inayokubalika na  Wateja wa ndani na nje ya Taasisi ili kuwafanya Wateja wao  kuwa huru kufikisha malalamiko yao bila ya kuwa na wasiwasi wa aina yeyote. Mavika ametoa kauli hiyo leo  jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo maalum yaliyofanyika  kwa muda wa  siku tatu kwa Waratibu wa Kushughulikia Mrejesho kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma. Mavika mewataka Waratibu hao kutoa  fursa sawa  kwa wananchi wote  kwa  kutumia mfumo wa  e-Mrejesho i...

Chuo Kikuu Kairuki chaweka msisitizo tiba zifanyike kidijitali

Na Mwandishi Wetu SPIKA mstaafu Anne Makinda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairuki amependekeza zifanyike tafiti kujua sababu za watoto wengi wa kiume kuachwa nyuma kitaaluma na wenzao wa kike. Aliyasema hayo jana wakati wa kongamano la sita kitaaluma lililoandaliwa na chuo hicho kujadili namna sekta ya afya inaavyoweza kufanya mabadiliko kwa huduma hizokutolewa kidijitali. Alisema kwa siku za karibuni watoto wa kike wameonekana kuongoza kitaaaluma na kuwaacha mbali wenzao wa kiume jambo ambalo alisema jamii haipaswi kulifumbia macho na kuliona kama la kawaida. “Hili si jambo la kawaida kabisa na tusilichukulie kirahisi lazima tutafute sababu za kwanini hawa watoto wanaanguka kitaaluma, lazima kuna sababu kwa hiyo tukifanya utaafiti tutapataa sababu na tutachukua hatua,” alisema Anne Makinda “Ni jambo jema kuona watoto wa kike wanakuwa mbele kielimu baada ya miaka mingi ya kuwa nyuma lakini siyo lengo letu kufurahia watoto wa kiume kuachwa nyuma, tuwapongeze watoto wa kike lakin...

Waziri Mkuu awataka Wahandisi Wazingatie Maadili

✅_Ataka vizuizi na vituo vya ukaguzi kuzingatia usalama wa watumiaji_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa awataka wahandisi wote nchini wazingatie miiko na maadili ya taalum hiyo ikiwemo kuitekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha halisi iliyotolewa. “Sote tunatambua kwamba wapo  wachache katika taaluma yenu ya uhandisi ambao wanaichafua kwa kufanya matendo ambayo ni kinyume na taaluma lakini pia ni kinyume na maadili.” “Matendo hayo ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, na ukosefu wa weledi. Hii si tu kwamba inachafua taaluma ya uhandisi, bali pia inaharibu taswira ya nchi”. Ameyasena hayo leo (Desemba 06, 2024) kwenye Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha. Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Bodi ya usajili wa Wahandisi isimamie maadili ya kihandisi na makampuni ya kihandisi kwa mujibu wa sheria ili kulinda hadhi ya uhandisi nchini. Waziri Mkuu ametoa rai kwa Taasi...