Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MNEC Assas Aeleza Mkakati wa CCM Katika Vituo 87,000 vya Kupigia Kura

Ruvuma.  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), Salim Abri Assas, ameweka wazi mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, akibainisha kuwa vituo vyote 87,000 vya kupigia kura nchi nzima vitakuwa na sanduku la kura, hata katika maeneo ambayo hayana wagombea wa vyama vya upinzani. Akizungumza katika mkutano wa kampeni mkoani Ruvuma, Assas alisisitiza umuhimu wa wanachama wa CCM kushiriki kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi. “Tutahakikisha kila kituo kina sanduku la kura, na pale ambapo hakuna wagombea wa upinzani, wapiga kura watapiga kura za ndiyo kuwachagua viongozi bora wa CCM,” alisema. Katika hotuba yake, Assas alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa wanachama wa CCM, akieleza kuwa mafanikio ya chama hicho yanatokana na juhudi za pamoja za wanachama wake. “Tunataka kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa wanadumisha misingi ya maendeleo na mshikamano wa kitaifa,” aliongeza. MNEC Assas alitumia fursa hiyo kuhimiza wananchi kuendelea kuamini katika CCM kama chama chenye...

Waziri Mkuu ameagiza Mitaala inayoandaliwa izingatie Mabadiliko ya Kiuchumi na Teknolojia

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kuwa mitaala inayoandaliwa ihakikishe inazingatia mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ya kiteknolojia. Amesema hayo leo (Ijumaa, Novemba 22, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la tano la Maendeleo ya Biashara na Uchumi linalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma. Amesema kuwa kuna umuhimu wa kutumia teknolojia katika kuboresha elimu ya biashara kwa kutumia jukwaa la mtandao kutoa mafunzo ya biashara, matumizi ya programu za kisasa za biashara, na kupanua matumizi ya teknolojia katika biashara na ujasiriamali. “Hivyo, nitoe rai kwa taasisi za elimu na mafunzo ya biashara kujikita katika matumizi ya teknolojia katika utoaji wa mafunzo” Pia, ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau waendelee kuimarisha na kuboresha mifumo ya elimu ya biashara katika ngazi zote za shule na vyuo na kuhakikisha inakidhi mahitaji ya soko la ajira. Katika Hatua nyingine, Mhes...

Wananchi wa Babati Wamshukuru Dkt. Samia kwa Kuwafungulia Barabara

Babati, Manyara Wananchi wa Kata ya Babati wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madaraja saba (7) pamoja na kufungua barabara katika kata hiyo ambapo kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata adha ya usafiri hususan kipindi cha mvua. Akitoa pongezi hizo Diwani wa kata ya Babati  Mhe. Haruni Msalu amesema kwamba wanamshukuru Rais kwa kuwatendea haki Kata ya Babati kwani Kata hiyo ilikuwa na makorongo mengi sana na kusababisha wananchi kuteseka hasa kipindi cha mvua na hivyo kusababisha kusimamisha kwa muda shughuli zao za kila siku. Amesema katika kipindi cha Awamu ya sita  Serikali kupitia TARURA imeweza kujenga madaraja yapatayo saba katika Kata ya babati katika eneo la Amboni C, Kambi ya Fisi, Hostel  ya chuo cha uhasibu na Old Majengo-Angoni. “Old Majengo kuja Angoni kulikuwa na kortongo kubwa ambalo lilikuwa likipitisha maji kwenda ziwani, wananchi wakiwemo wanafunzi walikuwa wakipata tabu sana na hivyo kuathiri utenda...

Waziri Mkuu Kufungua Kongamano la Maendeleo ya Biashara ya Uchumi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Novemba 22, 2024 anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la tano ya Maendeleo ya Biashara na Uchumi linalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma. Kongamano hilo linatoa fursa kwa wanafunzi, taasisi za elimu, wataalamu wa sera, wajasiriamali, na wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kujadili na kushauri kuhusu masuala yanayohusiana na mazingira ya biashara na uwekezaji.  Pia, Kongamano hilo linatoa fursa ya kutafuta suluhisho la changamoto za taaluma ya biashara na uchumi na kuongeza ufanisi katika mifumo ya biashara na uwekezaji ili kuongeza kasi ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii.

Jenerali Mstaafu Mabeyo apongeza Kasi ya Ujenzi wa Nyumba Msomera

 -Nyumba 2,500 Zakamilika Msomera,Usambazaji wa Umeme Wafikia asilimia 98,Miundombinu Mingine Mbioni Kukamilika.  Kassim Nyaki, Msomera Tanga. Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 21 Novemba, 2024  imefanya ziara ya kikazi kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro wanaoendelea kuhamia eneo hilo. Akiongoza bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) amezipongeza Sekta zote zinazohusika kutekeleza mradi huo kijiji cha Msomera kwa kukamilisha Nyumba 2500, ujenzi wa miundombinu ya Maji, mawasiliano, barabara, minada, majosho, kituo cha kuuzia maziwa, shule, zahanati, shule, kutenga maeneo ya malisho na miundombinu mingine kijijini hapo. "Tumetembelea eneo la Block F ambapo nyumba 1,000 zimekamilishwa katika awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa Nyumba 5,000, kitalu hiki pekee kuna matenki matatu ya maji yeny...

Bukombe wanataka Maendeleo na Maendeleo ni Ccm-Dkt.Biteko

*📌 Asema Vyama Vishindane kwa Sera na Utekelezaji wa Ahadi* *📌WanaCCM Bukombe Waaswa Kuimarisha Ushirikiano* *📌 Azindua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bukombe* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kwa miaka yote wananchi wa Wilaya ya Bukombe wamekuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kiu ya maendeleo. Amesema wananchi hao wana haki ya kuchagua kati ya maneno au maendeleo na  wamekuwa wakitamani maendeleo kwa kuwa na shule, barabara na zahanati. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 21, 2024  wakati akifungua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wilaya ya Bukombe zilizofanyika katika Kata ya Igulwa, Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita. “ Tunapozindua kampeni zetu tuna wajibu wa kuchagua maneno au maendeleo, tutashindanisha vyama kwa sera na kuonesha tuliyofanya kwa kipindi kilichopita. Tumekuja leo kuwaambia sisi tuko upande wa maendeleo na wengine wako upande wa maneno ...