Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais mwinyi awasili china

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akimbatana na Mke wake Mhe. Mama Mariam Mwinyi amewasili katika uwanja wa ndege wa Pudong International Airport, Shanghai, China akitokea Doha, Qatar na kupokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, China Mhe. Khamis Mussa Omar. Rais Dk. Mwinyi na ujumbe wake wanatarajiwa kuhudhuria ufunguzi wa Maonesho ya 7 ya China International Import Expo (CIIE) pamoja na kutembelea mabanda ya washiriki mbalimbali ya maonesho hayo.  Aidha, katika maonesho hayo Tanzania imepewa heshima maalum kuwakilisha bara la Afrika kutokana na mchango  mkubwa wa zaidi ya Kampuni 17 pamoja na sekta za kilimo, kazi za sanaa za mikono, bidhaa za kilimo na uchumi wa buluu.

Zingatieni misingi ya utawala bora katika usimamizi wa rasilimali watu-Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wasimamizi wote wa rasilimaliwatu wazingatie misingi ya utawala bora na weledi katika kuisimamia rasilimali hiyo katika Sekta ya Umma Barani Afrika. Amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha kutoa huduma bora na kudumisha imani ya wananchi kwa Serikali zao. Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Novemba 04, 2024) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Mwaka wa Mtandao wa Wasimamizi na Mameneja wa Rasilimaliwatu Katika Sekta ya Umma Barani Afrika (APS-HRMnet) jijini Arusha. “Rasilimaliwatu ina mchango mkubwa katika kuiwezesha Serikali kufikia malengo ya maendeleo iliyojiwekea pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Hivyo ninyi, kwa kuwa ni wataalam katika usimamizi wa Rasilimaliwatu mnao wajibu na dhamana kubwa ya kuhakikisha mnasimamia ipasavyo Rasilimali hiyo muhimu na ya thamani” Amesema kuwa ili kuimarisha  usimamizi wa kimkakati wa rasilimaliwatu na kukabiliana na changamo...

Waziri mkuu akutana na balozi wa Denmark nchini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 4, 2024 amefanya mazungumzo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jespper Kammersgaard, kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam

Bingwa Mathayo Cup 2024 kuondoka na zawadi ya ng'ombe na millioni moja

Na Shomari Binda-Musoma BINGWA wa mashindano ya Mathayo Cup 2024 jimbo la Musoma mjini  ataondoka na zawadi ya ng'ombe  na milioni moja. Jumla ya  timu 16 kutoka Kata za manispaa ya Musoma zinawanio zawadi hiyo na nyingine zitakazlkwa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.  Akifungua mashindano hayo baada ya kukabidhi jezi na mixpira kwa timu  shiriki mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma   Chikoka amesema  mbunge Mathayo amefanya  jambo kubwa katika kuinua michezo. Amesema mji wa Musoma unatakiwa kuchangamka kupitia matukio mbalimbali yakiwemo ya kimichezo   kama alivyofanya mbunge Mathayo. Chikoka amesema mashindano hayo yameonekana yatakuwa na ushindani kutokana na hamasa ya zawadi na maandalizi ya timu. " Nimshukuru sana mbunge Mathayo kwa kuanzisha mashindano haya yamekuja kuchangamsha mji wa Musoma. "Zawadi ni kubwa zilizoandaliwa na mbunge tukapambane na kucheza kwa nidhamu   katika kipindi chote cha mashindano",...

Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini akagua eneo la kuzikwa Musuguri kijijini butiama

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewasili nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri wilayani Butiama Mkoani Mara tarehe 03 Novemba 2024 kwa ajili ya kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kukagua maandalizi ya Mazishi ya Hayati Jenerali Musuguri yatakayofanyika tarehe 04 Novemba 2024. Jenerali Mkunda amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kuwashukuru wananchi wa Butiama na maeneo ya karibu kwa kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu  ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa taifa letu. Jenerali Musuguri aliyefariki tarehe 29 Oktoba 2024 akiwa na umri wa Miaka 104 atazikwa nyumbani kwake kwa heshima zote za kijeshi.

Waziri mkuu ahani msiba wa mzee Tutuba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 03, 2024 amehani msiba wa Mzee John Tutuba ambaye ni baba mzazi wa  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba nyumbani kwa Gavana huyo Oysterbay jijini Dar es salaam  Mzee Tutuba alifariki Novemba 01, 2024 katika Hospitali ya Shifaa Pan African ya Kinondoni jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa.