Bingwa Mathayo Cup 2024 kuondoka na zawadi ya ng'ombe na millioni moja

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma

BINGWA wa mashindano ya Mathayo Cup 2024 jimbo la Musoma mjini  ataondoka na zawadi ya ng'ombe  na milioni moja.

Jumla ya  timu 16 kutoka Kata za manispaa ya Musoma zinawanio zawadi hiyo na nyingine zitakazlkwa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.

 Akifungua mashindano hayo baada ya kukabidhi jezi na mixpira kwa timu  shiriki mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma   Chikoka amesema  mbunge Mathayo amefanya  jambo kubwa katika kuinua michezo.

Amesema mji wa Musoma unatakiwa kuchangamka kupitia matukio mbalimbali yakiwemo ya kimichezo   kama alivyofanya mbunge Mathayo.

Chikoka amesema mashindano hayo yameonekana yatakuwa na ushindani kutokana na hamasa ya zawadi na maandalizi ya timu.

" Nimshukuru sana mbunge Mathayo kwa kuanzisha mashindano haya yamekuja kuchangamsha mji wa Musoma.

"Zawadi ni kubwa zilizoandaliwa na mbunge tukapambane na kucheza kwa nidhamu   katika kipindi chote cha mashindano", amesema.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema kama waatibu watasimamia mashindano hayo kuhakikisha yanafanyika kwa ufanisi.

Amesema nidhamu ni muhimu kuzingatiwa kwa kila timu ili kuweza kufikia malengo kusudiwa ya mashindano hayo.

Michezo ya ufunguzi iliyofanyika novemba 3 Mwigobero ilifungwa bao 1-0 na Mukendo huku Iringo ikishindwa kufungana na Kitaji.

Mashindano hayo yataendelea leo kwa michezo miwili Kamnyonge dhidi ya Makoko na Mwisenge na Buhare



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top