Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Biteko akutana na ujumbe wa chama cha kikomunisti cha Vietnam

Naibu Waziri Mkuu Mhe.Dkt. Doto Biteko Leo Septemba 23, 2024 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kikao na Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam ukiongozwa na Mhe. Phan Dinh Trac kilichofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Biteko ameeleza kuwa Tanzania na Vietnam zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na zinaendelea kuimarisha uhusiano huo katika nyanja za diplomasia, siasa na uchumi.  Aidha, ameipongeza Vietnam kwa kufanya uwekezaji nchini Tanzania ikiwemo katika Kampuni ya Simu za Halotel na kusema kuwa nchi hizo zinahitaji kuongeza kiwango cha biashara kati yake ambapo kiwango cha uwekezaji kwa sasa ni dola za kimarekani milioni 300. Kwa upande wake, Mhe. Trac ameipongeza Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvutia uwekezaji, kuboresha huduma za afya, sambamba na kupiga vita vitendo vya rushwa. Ameongeza kuwa, kufuatia jitihada hizo kiwango cha ukuaji uchumi k...

Waziri Pindi Chana Awaomba Machifu Kuelimisha Jamii Umuhimu wa Umoja na Amani

Na Elizabeth Cornely WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amewaomba Machifu kutoka maeneo mbalimbali nchini kuelimisha Jamii Umuhimu wa umoja, amani na mshikamano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Waziri Chana ametoa kauli hiyo mjini Songea alipozungumza na Machifu hao walioshiriki katika Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalohitishwa leo mkoani Ruvuma. Amesema viongozi hao wa kimila wana mchango na nguvu kubwa ya kuhubiri umoja na amani kwa wananchi wao hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye chaguzi. "Leo hii nchi yetu ina utulivu na amani kwa sababu miongoni mwa watu waliochangia kufanikisha hilo ni Machifu pamoja na viongozi wa dini, tunaomba muendelee kufundisha kizazi cha sasa na kijacho mila na desturi za nchi yetu,"amesema Waziri Chana. "Tukumbuke tuko kwenye maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, kwa hiyo kwanza tuhamasishe watu wagombee lakini kulinda umoja na amani ya nchi yet...

Tanzania Kuimarisha zaidi Usalama wa Kwa Njia ya Maji Kuimarisha Uchumi

Na Shomari Binda-Musoma TANZANIA imekusudia kuimalisha zaidi usalama wakati wa matumizi ya usafiri majini kwenye bahari na ziwa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ( SMZ ) Khalid Muhamed Salum kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Majj Duniani na miaka 50 ya uanachama wa IMO. Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Makame Haji kwenye ufunguzi uliofanyika kitaifa leo septemba 23 uwanja wa shule ya msingi Mukendo. Amesema suala la usalama lina umuhimu mkubwa na kutaka maadhimisho hayo yatumike kukumbushana na kuzingatia usalama. Makame amesema Tanzania kama nchi mwanachama wa Mamlaka ya Bahari Duniani ( IMO ) inazingatia mkataba wa mamlaka hiyo na usalama unasisitizwa. Amesema usafiri wa majini ni moja ya usafiri unaotegemewa hivyo ni muhimu wananchi kupata elimu juu ya usalama. " Hii ni siku muhimu kupitia maadhimisho haya kukumbushana suala la usalama tunapotumia vyombo vy...

Wananchi Wafurika Uwanja wa Majimaji Kumsikiliza Rais Dkt. Samia

Katika hali ya hamasa kubwa, umati mkubwa wa wananchi wa Mji wa Songea umejitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Majimaji, kumshuhudia na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 23 Septemba 2024  katika kilele cha Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni, lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mkoani Ruvuma. Mhe. Rais Dkt. Samia ni mgeni rasmi wa tamasha hilo, lililojikita katika kuonesha na kusherehekea utajiri wa urithi wa kitamaduni wa Tanzania.  Kabla ya hotuba yake, Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya utamaduni, ambapo alijionea kazi mbalimbali za sanaa na utamaduni, na hata kushiriki kucheza mchezo wa bao, jambo lililowafurahisha wananchi na wasanii waliokuwepo. Shughuli hiyo inaendelea kwa shamrashamra, huku wananchi wakionesha shauku na furaha kubwa kwa ziara ya Rais katika eneo hilo, likiwa na umuhimu mkubwa kwa historia na utamaduni wa taifa...

Rais Dkt. Samia Atembelea Makaburi ya Mashujaa Waliopigania Uhuru Katika Vita ya Maji Maji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu akiwa kwenye picha za matukio mbalimbali pamoja na Machifu wa Ruvuma, pia akitoa heshima kwenye makaburi ya mashujaa waliopigania uhuru katika vita ya majimaji alipotembelea katika makumbusho ya mashujaa.

Serikali yatangaza bei elekezi ya mahindi mkoani ruvuma

Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe ametangaza bei elekezi ya kununua mahindi Mkoani Ruvuma, kuwa kilo moja ya mahindi itauzwa kwa bei isiyo pungua shilingi 550 kwa kilo moja. Waziri Bashe amesema hayo alipokuwa anazungumza na maafisa kilimo, wafanya biashara ya mazao,mbegu na mbolea, maafisa ugani na wadau wengine wa kilimo; wilayani Songea.  Katika mkutano huo,Waziri Bashe amesisitiza umuhimu wa kufuata bei elekezi na kwamba wataalamu wa wizara watapita vijijini na wilayani kusajili mawakala ili kuhakikisha biashara ya mahindi inafanyika kwa ufanisi. Waziri Bashe amebainisha kuwa serikali inapotoa bei elekezi, inazingatia uhalisia wa soko, gharama za uzalishaji na gharama nyinginezo.  Ameomgeza kuwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi wanaotaka kununua mazao lazima wapitie kwa wafanyabiashara wa ndani. "Tenengenezeni umoja wenu wenye nguvu na serikali ipo tayari kufanya kazi na nyie,”alisema Bashe.  Alifafanua kuwa wafanyabiashara wanaonunua mahindi kwa niaba ya WFP walikuwa ...