Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Yafunga Mwenendo wa Kesi ya Mauaji ya Mtoto Noela

Na Angela Sebastatian- Bukoba MAHAKAMA ya hakimu mkazi Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imefunga rasmi mwenendo kabidhi kuhusu shauri namba 17740  linalowakabiri washitakiwa tisa akiwemo padri wa kanisa Katoliki pamoja na baba mzazi wa mtoto Noela Asimwe Novart (2.5) ambaye aliuawa na kisha kukatwa mikono yako na mwili kutelekezwa katika karavati. Waziri Magumbo mwendesha mashitaka wa mkoa wa Kagera kwa kushirikiana wa mawakili wenzake wanne wa serikali akiwemo Erick Mabagala  alisema kuwa kesi hiyo  ilifikishwa mbele ya hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya wilaya Bukoba Elipokea Yona kwa mara ya kwanza Juni 28 mwaka. Amesema Mei 30 mwaka huu mtoto Noela aliibwa na watu wasiojulikama ambao walifika nyumbani  kwao marehemu huyo na kumpola mikononi mwa mama yake kisha kutokomea kusikojulikana ambapo Juni 17mwaka huu mwili wa Noela ulipatikana ukiwa umetelekezwa katika karavati lililoko barabara ya Ruhanga ukiwa umekatwa mikono. Magumbo akisaidiana mawakili wanne wa Jamhuri ...

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA MAENDELEO BANK

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 07, 2024 ameshiriki katika mbio za hisani za Maendeleo Bank Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia katika viwanja vya Greenpark garden Oysterbay jijini Dar es Salaam. Lengo la mbio hizo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye changamoto mbalimbali hapa nchini. Kauli mbiu ya mbio hizo ni “Hatua ya Faraja- Msimu wa Pili”.

Wanawake Wahimizwa Kujitokeza Kwenye Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura Kuhakiki Taarifa Zao

Na Shomari Binda-Musoma WANAWAKE mkoa wa Mara wametakiwa kujitokeza kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga Kura kwa ajili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Kauli hiyo imetolewa Leo Septemba 6, 2024 na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake wa ( UWT) Taifa Rhobi Samwelly alipokuwa akizungumza na George Marato TV. Amesema siku zote wanawake wamekuwa mstari wa mbele kwenye masuala mbalimbali yakiwemo ya uchaguzi. Rhobi amesema katika zoezi hili la uboreshaji wa daftari kwa mkoa wa Mara lililoanza septemba 4 hadi 10 wanawake wote wenye sifa wanapaswa kujitokeza kushiriki zoezi hilo. Mjumbe huyo wa baraza la UWT Taifa amesema wanawake wasisubiri hadi siku ya mwisho bali wajitokeze sasa kujiandikisha na kuboresha taarifa. Amesema bila kujiandikisha na kuboresha taarifa huwezi kushiriki kikamilifu zoezi la uchaguzi pale litakapofika. " Zimebaki takribani siku chache kuhitimisha zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura kwenye mk...

Wananchi Nyatwali Wamuahidi Rc Mtambi Matumizi Sahihi ya Fedha za Fidia

Na Shomari Binda- Bunda WANANCHI wa  Kata ya Nyatwali wilayani Bunda  wamemuahidi mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambj matumizi sahihi ya fedha za fidia kupisha shughuli za uhifadhi. Ahadi hiyo wameitoa kwenye Kata hiyo wakati wakipokea mfano wa hundi ya malipo hayo yanayotolewa na serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) Wamesema fedha watakazolipwa watazielekeza kwenye kupata makazi mapya na kuweka mazingira mazuri ya maisha kwenye maeneo watakayoamia Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Nzugumi Mayala amesema ushauri wa mkuu wa mkoa wataufanyia kazi baada ya kupata fedha hizo. Mkuu wa Mkoa  wa Mara Kanali Evans Mtambi amezindua ulipaji fidia kwa wananchi wanaohamishwa kutoka kata ya Nyatwali wilayani Bunda. Akizindua ulipaji wa fidia hizo katani hapo RC Mtambi amewataka wananchi wanaopata malipo hayo kuondoka katika eneo hilo na kutumia fedha hizo vizuri kwa maslahi ya familia zao. “Akili zenu zianze kufikiria jinsi mtakavyopata faida ku...

Wizara ya Katiba na Sheria Yazindua Rasmi Kituo Cha Huduma Kwa Mteja

  Na Elizabeth Zaya WIZARA ya Katiba na Sheria, imezindua rasmi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Huduma za Kisheria ambacho kitakuwa kinapokea malalamiko, hoja maswali na tuhuma za rushwa kwa njia ya simu kutoka kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na kutatuliwa moja kwa moja na wataalamu. Kituo hicho kimezinduliwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, hafla iliyoshirikisha viongozi  wadau mbalimbali pamoja na wananchi na kwamba kituo hicho ni sehemu ya Kampeni ya Kitaifa ya Huduma za Kisheria ya Mama Samia. Prof.Kabudi alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni miongoni wiazara  vinara  zinazotekeleza kwa vitendo falsafa za Rais Samia Suluhu Hassan za 4R, ambazo ni maridhiano, ustahilmilivu, mabadiriko na kujenga upya. “Na kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, imefanikiwa kupita katika mikoa saba na hivi karibuni itaanza kuendelea katika mikoa mingine iliyobaki,”alisema Prof.Kabudi. Amesema wizara imeanzisha kitu...

Rais Dkt. Samia Akutana na Watanzania Wanaoishi Nchini China

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Watanzania wanaoishi nchini China (Diaspora) wakiwemo wafanyakazi, wanafunzi na wafanyabiashara,  Jijini Beijing tarehe 06 Septemba, 2024.