Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Emmanuel Nchimbi Awasili Kigoma Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewasili mkoani Kigoma tayari kuanza ziara ya mikoa mitano ya Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Mwanza  Balozi Nchimbi amewasili leo asubuhi Agosti 4, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Ndg. Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni, pamoja na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.  Baada ya kutua, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi pamoja na ujumbe wake amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa huo,tayari kwa  kuanza ziara ya siku 3 mkoani humo.  Malengo ya ziara hiyo ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhamasisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Wakaazi kwa ajili ya maandalizi ...

Rais Mwinyi Afungua Maonesho ya Nane Nane Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa kukifanya kilimo biashara chenye tija kwa kuimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi kwa mlaji. Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 3 Julai 2024 alipofungua maonesho ya saba ya kilimo ya Nane Nane Zanzibar katika viwanja vya Dole , Kizimbani Mkoa wa Mjini. Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaanzisha vituo maalum kila wilaya kuhamasisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima na wafugaji nchini.  Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali inatarajia kutekeleza mradi mkubwa  wa mageuzi wa uzalishaji wa wafugaji wa maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo ambao utazingatia mabadiliko ya tabia nchi yenye gharama za  shilingi bilioni 7.5. Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mifugo kwa kujiajiri , pia amewahimiza wajifunze mbinu bora za kilimo na ufugaji kupitia maonesh...

Rais Dkt. Samia Azindua Bwawa la Umwagiliaji Katika Kiwanda Cha Sukari Cha Mtibwa

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua Bwawa la umwagiliaji lenye mita za ujazo milioni 25 pamoja na Awamu ya tatu ya upanuzi wa mashamba na umwagiliaji katika Kiwanda cha Sukari Mtibwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya Kikazi, Mvomero Mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti, 2024. Matukio mengine Katika Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mara baada ya kuzindua Bwawa la umwagiliaji lenye mita za ujazo milioni 25 pamoja na Awamu ya tatu ya upanuzi wa mashamba ya Kiwanda hicho, Mvomero Mkoani Morogoro.

SGR Yaongeza Idadi ya Watalii Nchini

Na Zainab Ally-Mikumi. Ikiwa ni Siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kuzindua Reli ya Mwendokasi (SGR) watalii ambao ni watumishi wa kada ya ualimu zaidi ya 1000 kutoka mkoa wa Dar es Salaam wametumia usafiri wa reli hiyo kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi. Ziara hiyo iliyoratibiwa na Ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam imelenga kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Samia ikiwemo kutangaza vivutio vilivyopo Hifadhi za Taifa ambapo kwa umoja wao walichagua Hifadhi  ya Taifa Mikumi lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia. Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Dkt. Toba Nguvila, amesema kuwa watalii hao ambao ni walimu wa mkoa wa Dar es Saam wameamua kuchangisha fedha zao wenyewe kwa ajili ya kuja kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa kutumia usafiri wa reli ya kisasa ya SGR lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Samia. “Baada ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kuizindua reli hii, walimu wa mkoa wa Dar es Salaam w...

Taarifa ya Wizara ya Afya Kuhusu Ugonjwa Wa MPOX

  🟩 Mpaka sasa Tanzania ni salama na hakuna mgonjwa yoyote aliyepatikana na ugonjwa huo.   🟩 Ugonjwa wa Mpox unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo; kupitia maji maji ya mwili ikiwemo mate, matapishi, jasho, mkojo, matone ya mfumo wa njia ya hewa na ngozi kupitia kugusana na kujamiana na mtu mwenye maambukizi ama kutumia vifaa, matandiko au kugusa sehemu zilizo na vimelea vya ugonjwa huu. Aidha, ugonjwa huu unaweza pia kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.   🟩 Dalili kuu ya Mpox ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa, mikono na miguu, kifuani, usoni na wakati mwingine sehemu za siri. Dalili nyingine ni homa, uchovu, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mitoki.    🟩 Ugonjwa huu haujaingia nchini, hivyo, ni vyema tukashirikiana kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salama. Wizara inatoa tahadhari kwa Wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa huu kwa k...

Mwambukusi Ashinda Urais TLS 2024/2027

Boniface Mwambukusi ameshinda nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) 2024/2027 Kwa kura 1,274