Na Mwandishi wetu Jovina Massano.
Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania(UWT) wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara wamtunuku tuzo ya heshima Mbunge wa viti maalum Agnes Marwa kwa kuendelea kukijenga chama.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Godfrey Kavenga Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mara kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mara Nansi Msafiri katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya umoja huo kimkoa yaliyofanyika katika eneo la chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma.
Nansi amesema UWT imeona na kutambua jitihada zinazofanywa na mbunge huyo za kuhakikisha chama kinaendelea kuimarika kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa.
Kilele hicho kimefanyika Oktoba 4,2026 ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo ya UWT Rorya na jengo la UWT lililopo Kata ya Mwisenge .
Mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mbunge Agnes amewashukuru viongozi wote wa chama na wa Jumuiya ya wanawake kwa zawadi hiyo.
Mbali na shukrani hizo hakusita kuwashauri wanachama kuendelea kukijenga chama na kuacha kupigana kwa maneno kwa kuwa msingi wa chama ni umoja,amani, Upendo na mshikamano.
" Tupo ndani ya Chama kujenga kila mmoja anatakiwa ashiriki kuhakikisha chama kinakuwa imara kuanzia ngazi ya chini hivyo tusipiganishe chama tukijenge", amesema Mbunge Agnes.
Ameongeza kuwa ni wote ni wanaCCM hakuna haja ya kupigana vita pia ni muhimu ukiona juhudi anazofanya kiongozi mwenzio nawe ongeza juhudi ili chama kiendelee kuwa imara zaidi pia amezisisitiza kujikita kwenye maendeleo na kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya chama unafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Tuzo hiyo imembatana na zawadi ambayo UWT imekabidhiwa wa Mbunge Agnes na mwenza wake.
Nae Katibu wa CCM Mkoani Mara Godfrey Kavenga amewapongeza UWT na wanachama wote na kuwaeleza kuwa yupo tayari kushirikiana na wanaCCM yeyote na yupo tayari kupokea ushauri na maoni yenye kujenga kwa mustakabali wa chama.
Kwa Upande wake mjumbe wa Baraza kuu la UWT Taifa ngazi ya viti vitano Tanzania bara Mariam Sagini amempongeza Mbunge huyo kwa kuendeleza mshikamano kwa wanachama.






Comments
Post a Comment