Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) haijaridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhusu hoja zilizojitokeza katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Agosti 18,2026 Bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Devotha Minja amesema Kamat
Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG, Chuo hicho kilifanya manunuzi ya shilingi bilioni 29.77 ambazo zilitolewa na wazabuni wasiokidhi vigezo na shilingi bilioni 1.54 zilizotolewa kwa watu wasiokidhi viwango.
Aidha, alisema Kamati haijaridhishwa na ujenzi wa barabara chini ya kiwango yenye thamani ya shilingi milioni 523 pamoja na madai ya ziada ya shilingi milioni 718 ambayo hayastahili na hayakuzingatia masharti ya mkataba.
Mheshimiwa Devotha amesema Kamati inatafakari hatua zaidi za kuchukua ili kulishauri Bunge ipasavyo.
Kamati ya PAC ilikuwa inajadili Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu cha Mzumbe.



Comments
Post a Comment