Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Moto mkubwa uliozuka majira ya saa mbili usiku umeteketeza maduka 11 na nyumba 2 eneo la standi ya daladala Barabara 12 jijini Tanga.
Akizungumza baada ya tukio hilo mmiliki wa nyumba Mzee Hamisi Abdallah amesema moto huo umesababisha hasara kubwa kwani hawaja wafanikiwa kuokoa kitu chochote zaidi ya roho zao.
Aidha Hamisi pia ameiomba serikali kumuangalia Kwa hicho la tatu kwani tukio hilo limemridisha nyuma kiuchumi na kwamba hilo ndilo lilikiwa tegemeo kubwa kwake.
Kwa Upande wake mmiliki wa maduka mawili ambaye pia ni muhanga wa moto huo Godias Anthony Kimath amesema mpaka sasa ameshaukaribisha umasikini wakasi na hivyo anajipanga namna ya kusimama tena kwani mali zinatafutwa.
"Nilikuja Tanga nikiwa Sina kitu hivyo basi Sina budi kumshukuru mungu Kwa tukio hili na kikubwa ni kujipanga na kuangalia namna gani nitasimama tena japo hasara ni Kubwa sana kwani sijaokoa kitu chochote,"alisema Kimath




Comments
Post a Comment