Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde leo tarehe 21.08.2026 Jijini Dodoma amekutana na kujadiliana na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Saudi Gold Refinery Ndg. Faisal Alothaim juu ya mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya Madini nchini Tanzania.
Mh. Mavunde amewahakikishia wawekezaji hao kwamba serikalinya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini Tanzania na uwepo wa madini mengi nchini Tanzania unatoa fursa kwa wigo mpana wa eneo la uwekezaji.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Saudi Gold Refinery Ndg. Faisal Alothaim ameshukuru Tanzania kwa maandalizi mazuri ya Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Saud Arabia ambalo limefungua fursa kubwa ya ushirikiano kupitia nchi hizi mbili.
Ameongeza kwamba,Tanzania ni kati ya nchi zenye mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba Kampuni yake ipo tayari kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Madini kwa kufanya utafiti wa kina na baadaye uwekezaji mkubwa wa u uchimbaji wa madini kwa mujibu wa Sheria za nchi.





Comments
Post a Comment