Na Mwandishi wetu Jovina Massano
BAADHI ya wazazi na walezi Manispaa ya Musoma wahamasika watoto wao kupata chanjo ya polio awamu ya tatu inayotarajia kuanza Agosti 27,2026.
Maria Kimario mkazi wa mtaa wa Sokoine Kata ya Mukendo amewapongeza waratibu, wahamasishaji na vyombo vya habari kwa kuweza kutoa taarifa kwa wakati.
Amesema wahamasishaji na viongozi wa mitaa wameweza kuwafikia na kuwapa elimu ya umuhimu wa chanjo hiyo lakini pia taarifa ya chanjo hiyo inaonekana kwenye vyombo vya habari.
"Elimu na taarifa zinapotolewa mapema husaidia wazazi na walezi kujiandaa na kuitikia kwa wingi na kuwaepusha watoto kupooza kwa ghafla"amesema Maria.
Pia ameiomba viongozi kuwa na utaratibu wa kutoa elimu za masuala mbalimbali yanayoihusu Jamii ili kuondoa migongano isiyo ya lazima.
Eliza Sryvesta mkazi wa Mtakuja B kata ya Mwisenge amesema kuwa chanjo hii ni Muhimu kwa kuwa hivi sasa imepunguza magonjwa ya polio,ulemavu kwa watoto.
Ameongeza kuwa watoto wenye ulemavu miaka ya Sasa yamepungua si kama ilivyokuwa kipindi Cha nyuma watoto wengi walipata hali ya kupooza.
Amewashauri wazazi na walezi Wasipuuze kwa kuwaweka watoto ndani na kuacha kuwapa chanjo hiyo kwa kuwa ni salama na nzuri kwa watoto wetu.
"Wahamasishaji wakiwemo wenyeviti wa mitaa wameweza kufika na kutuhimiza,kutuelimisha umuhimu wa chanjo hii" amesema Eliza.
Kwa Upande wake Mratibu wa Chanjo ya Polio wa halmashauri ya Manispaa ya Musoma Jamila Hassan amewashikuru wazazi hao kwa kutambua umuhimu wa chanjo kwa kuwakumbusha wenzao kushiriki kikamilifu.
Ameeleza kuwa hatua wamezifanya za awali wameweza kuwapa mafunzo watoa huduma watakaokwenda kutoa chanjo hiyo Sambamba na timu ya uhamasishaji ambayo imewahusisha wenyeviti wa mitaa,watoa huduma ngazi ya Jamii (CHW).
"Ili jamii iweze kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la kutoa chanjo elimu na hamasa zinatolewa kupitia timu hizo katika maeneo yetu lengo nl kushirikiana kikamilifu kufanikiwa kufikia watoto tarajiwa wapatao 66,176 katika Manispaa hii na kuzuia wasipate maambukizi ya Polio,"amesema Jamila.
Nae mhamasishaji Agape John Salikoki amewakumbusha wazazi kuwa chanjo hii inawahusu watoto wote waliopata chanjo ya kwanza na ya pili.
Uhamasishaji utafanyika katika mitaa yote, Kata kwa kata na mashuleni ikiwemo nyumba za Ibada na taarifa kupitia vyombo vya habari ili kuwe na mwitikio mkubwa.
Amewaomba wazazi na walezi kutoa ushirikiano ili wote waweze kupata chanjo hii na kuwakinga watoto na ugonjwa huu wa kupooza kwa ghafla.
Chanjo hii imeanza kutolewa kwa awamu tofauti kuanzia mwezi Machi kwa awamu ya kwanza na ya pili mwezi Mei na ya tatu Agosti 27 hadi 30.




Comments
Post a Comment