Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

PROF. MKENDA: VETA ITOE UJUZI UNAOKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA


 WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezitaka Kamati za Ushauri wa Stadi (Training Advisory Committees–TACs) za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwa chachu ya kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na uzalishaji nchini.

Prof. Mkenda amesema kamati hizo zinapaswa kuwa kiungo madhubuti kati ya VETA, Serikali, waajiri na sekta binafsi, ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanakuwa na ujuzi, umahiri, ubunifu na uwezo wa kutumia teknolojia unaohitajika katika maeneo ya kazi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda Ameyasema hayo leo, Agosti 13, 2026, jijini Dodoma, wakati akizindua rasmi Kamati za Ushauri wa Stadi za VETA, ambapo amesisitiza kuwa mfumo wa mafunzo ya ufundi stadi haupaswi kuishia katika kutoa vyeti pekee, bali unapaswa kuwaandaa wahitimu kwa ajira, kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji.

“Hatupaswi kuwa na mfumo wa mafunzo unaoishia katika kutoa vyeti pekee. Tunataka kuwa na mfumo unaozalisha watu wenye ujuzi, umahiri, ubunifu, nidhamu ya kazi na uwezo wa kutumia teknolojia katika kuongeza tija na ushindani,” amesema Prof. Mkenda.

Amesema wajumbe wa TACs wana nafasi ya kipekee kwa kuwa wako karibu na mabadiliko ya teknolojia, uzalishaji na mahitaji ya waajiri, hivyo wanapaswa kuishauri VETA kwa wakati kuhusu stadi mpya zinazohitajika na mabadiliko yanayopaswa kufanyika katika mitaala.

Prof. Mkenda amewataka wajumbe hao kutokuwa kamati za mikutano pekee, bali kuwa “Kamati za Matokeo” kwa kubaini mapema mabadiliko katika sekta mbalimbali na kutoa ushauri unaoweza kusaidia VETA kuboresha programu za mafunzo.

Amesema ushauri wa kamati hizo unaweza kuamua iwapo kijana anayehitimu atakuwa na ujuzi unaohitajika katika eneo la kazi au kubaki na cheti kisichokidhi mahitaji ya mwajiri.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, maeneo yenye fursa kubwa ambayo yanahitaji kupewa kipaumbele katika mafunzo ni pamoja na ukarimu, utalii, sanaa, TEHAMA, uzalishaji, ujenzi, nishati na kilimo.

Prof. Mkenda amesema kuanzishwa kwa TACs kunakuja wakati Tanzania ikiwa katika hatua muhimu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inaweka mkazo katika kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani pamoja na kuongeza uwezo wa watu na maendeleo ya jamii.

Amesema utekelezaji wa Dira hiyo hauwezi kufanikiwa bila kuwa na nguvu kazi yenye maarifa, ujuzi na uwezo wa kutumia teknolojia na ubunifu.

“Hatuwezi kuwa na uchumi imara, jumuishi na shindani bila kuwa na watu wenye ujuzi. Hatuwezi kujenga viwanda vya kisasa bila kuwa na mafundi, mafundi sanifu, wataalamu wa teknolojia na watu wenye uwezo wa kuendesha na kutengeneza mifumo ya kisasa,” amesema.

Aidha, amesema Tanzania haiwezi kujenga uchumi wa kidijitali bila vijana wenye ujuzi wa TEHAMA, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa na huduma kwa kutumia maarifa, teknolojia na ubunifu wa ndani.

Waajiri watakiwa kushiriki katika mafunzo

Prof. Mkenda amewataka waajiri na sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika mfumo wa mafunzo ya ufundi stadi kwa kueleza aina ya ujuzi, teknolojia, vifaa na viwango vya utendaji vinavyohitajika katika maeneo ya kazi.

Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za elimu na sekta ya viwanda kupitia Mpango wa Kitaifa wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Sekta ya Viwanda katika Ukuzaji wa Ujuzi na Uwezeshaji wa Ajira, uliozinduliwa Februari 9, 2026, jijini Dar es Salaam.

Amesema mpango huo unalenga kuoanisha mafunzo na mahitaji halisi ya soko la ajira pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za elimu na sekta ya uzalishaji.

Kwa upande mwingine, amewataka wajumbe wa TACs kuwa mabalozi wa VETA katika sekta wanazotoka kwa kuwahamasisha waajiri kushirikiana na taasisi hiyo katika kuandaa mitaala, kutoa mafunzo kwa vitendo, kuboresha teknolojia na kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi unaohitajika.

Prof. Mkenda amesema mafunzo ya ufundi stadi yanapaswa pia kutoa fursa sawa kwa vijana, wanawake, watu wenye mahitaji maalum na makundi mengine yenye uhitaji wa fursa za kiuchumi.

Ameongeza kuwa jukumu hilo linaendana na Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, inayosisitiza kuwa mfumo wa elimu na mafunzo uzalishe watu wenye maarifa, ujuzi na umahiri unaokidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa na soko la ajira.

Prof. Mkenda amewataka wajumbe wa TACs kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi, ubunifu, uwajibikaji na uzalendo, akisisitiza kuwa Serikali inawategemea katika kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa mafunzo ya ufundi stadi.

“Kwa pamoja, tuhakikishe kwamba TACs zinakuwa chachu ya mabadiliko, daraja kati ya elimu na ajira, na injini ya ubora, ubunifu na ushindani wa Taifa,” na natamka kuwa nimezindua rasmi Kamati za Ushauri wa Stadi za VETA. Amesema



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...