Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga
Mfumo wa maktaba mtandao umekuwa na matokeo chanya kwa bodi ya huduma za maktaba kwani utarahisisha kusomana na mifumo mingine kama anavyosisitiza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kuhusu mifumo kusomana na tayari ndani yake kuna mifumo kadhaa ya kiserikali kama mfumo wa malipo ya serikali,madeni ya serikali na mingineyo,pia mifumo ya elimu kama mfumo wa takwimu ambao upo chini ya wizara ya elimu.
Hayo yamebainishwa na Mkurungenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Dkt. Mboni Ruzegea alipokuwa akitolea ufafanuzi juu ya kuanzishwa Kwa Maktaba mtandao na kuanza kufanya kazi kwake alipokuwa katika viwanja vya usagara yalipouwa yakifanyika maonesho ya kitaifa ya wiki ya elimu ujuzi na ubunifu.
Ruzegea pia amewataka watunzi wa vitabu au majarida kuhakikisha wanafika katika Maktaba kuu ya taifa na kuatiwa namba ya utambulisho,na katika machapisho hayo atatakiwa kuacha kopi mbili ila kwakuwa sasa tupo katika kipndi cha dijitali atatakiwa kupeleka soft copy Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu hiyo katika Maktaba ya taifa.
Sambamba na hayo pia Ruzegea amongeza kuwa wanatarajia kufanya kongomano kubwa la huduma za maktaba ambalo lilikuwa likifanyika kila mwaka japo lilisima kwa miaka miwili na kwamba katika kongomano hilo wanatarajia kufanya urasimishaji wa maktaba mtandao na sio uzinduzi kwani tayari huduma hiyo inatumika.
Kwa Upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo Cha ukutubi na uhifadhi nyaraka Bertha Mwaihojo amewakaribisha wanatanga na watanzania Kwa ujumla kujiunga na chuo hicho na kwamba ni miongoni mwa vyuo vikongwe nchini.
Mwaihojo pia alisema chuo hicho cha ukutubi na uhifadhi nyaraka kinaendeshwa na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ambapo hutoa mafunzo katika ngazi ya cheti na stashaha katika kozi za ukutubi na uhifadhi nyaraka pamoja na utunzaji wa nyaraka,huku kozi nyingine mpya zikitarajiwa kuanza mwaka huu wa masomo ambazo ni ICT na Business Information Technology.
Mwaihojo alimalizia kwa kusema kuwa mpaka sasa chuo hicho kina kampasi mbili hapa nchini ambazo ni Bagamoyo na Dar es salaam pekee.
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) ni taasisi ambayo ipo chini ya wizara ya elimu na imeanzishwa kisheria kazi yao kubwa ni kutoa huduma za maktaba kama usambazaji wa machapisho na vifaa vya machapisho kwa kutumia mfumo wa kuletwa kwa machapisho kisheria.






Comments
Post a Comment