Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana leo Julai 21, 2026 kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya.
Mara baada ya kuwasili, Rais Samia alipokea heshima ya wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kukagua gwaride rasmi la heshima lililoandaliwa kumkaribisha, ikiwa ni sehemu ya mapokezi ya viongozi wa nchi na serikali wanaoshiriki mkutano huo muhimu unaolenga kujadili masuala ya afya barani Afrika na kuimarisha ushirikiano wa nchi wanachama katika sekta hiyo.









Comments
Post a Comment