Undp Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida Yatoa Mafunzo Kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini

GEORGE MARATO TV
0


Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imeendelea kutoa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini yenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu uchimbaji salama, wenye tija na unaozingatia utunzaji wa mazingira.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea wachimbaji wa Mkoa wa Singida uwezo katika matumizi ya teknolojia bora za uchimbaji, usimamizi wa afya na usalama migodini, uongezaji thamani wa madini pamoja na kuimarisha shughuli za biashara ya madini kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo.

Awali akifungua mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida ,Afisa Madini Mkazi  wa Mkoa wa Singida Mhadisi  Sabai Nyansiri amesema kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo ili kuhakikisha sekta ya madini inakuwa chachu ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top