Waziri Kombo Asisitiza Ufanisi na Uadilifu kwa Watumishi wa Wizara

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amewasisitiza watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi, uadilifu na kufuata sheria, Kanuni na miongozo ya utumishi wa umma.

Amesema hatua hiyo itaendelea kukuza weledi katika kazi kwa watumishi wa wizara, na hivyo kujenga na kuimarisha taswira  ya wizara ndani na nje ya nchi.

Waziri Kombo ametoa rai hiyo alipokutana na watumishi wa wizara katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.











“Leo tumekutana wote kwa mara ya kwanza, watumishi wenzangu hamna budi kufanya kazi kwa ufanisi na mzingatie maadili na kufuata sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kujenga na kuimarisha taswira ya Wizara yetu ndani na nje ya Nchi na kulinda maslahi mapana ya nchi” alisema Mhe. Waziri.

Amebainisha kuwa watumishi wana dhamana kubwa ya kusimamia na kutekeleza diplomasia ya uchumi, jambo linalohitaji uzalendo katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya wizara.

Mhe. Kombo amesema ni muhimu watumishi kuondokana na dhana ya kufanya kazi kwa mazoea kwani nyakati hizi haziendani na dhana hiyo, huku akisisitiza Watumishi 

katika sehemu ya kazi kujiendeleza kitaaluma  na ili kumudu kasi ya  mabadiliko na hivyo kuiwezesha Wizara kufikia malengo ambayo imejiwekea. 

“Hizi ni zama za AI-Akili mnemba, kila mmoja anapaswa kujituma , kujiongeza na kujiendeleza ili kuendana na mahitaji ya wakati huu tuliopo na hivyo  kufikia malengo ya kimkakati ambayo wizara imejiwekea,” alisisitiza Mhe. Waziri.

Katika kikao hicho Mhe Waziri Kombo amewapongeza Watumishi wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kuwasihi kuendelea na moyo huo.

Kuhusu mazingira ya kazi, Mhe. Waziri Kombo amehimiza ushirikiano na mshikamano miongoni mwa watumishi wa kada zote,  kufanya kazi kama timu moja  ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa urahisi.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top