Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Ndomba Doran aliyeongozana na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.




Comments
Post a Comment