Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tuhakikishe Vijana Wanapata Mafunzo ya Ufundi Stadi-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa wazazi na walezi kote nchini kuhakikisha wanawapeleka vijana wao kupata mafunzo ya ufundi stadi yanayoratibiwa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuwawezesha kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri na kuchangia maendeleo ya Taifa. Akizungumza mara baada ya kukagua karakana za kujifunzia zilizopo katika Chuo cha VETA wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha miundombinu ya vyuo vya ufundi stadi pamoja na kuratibu programu za mafunzo ili kuhakikisha vijana wanapata stadi zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira la sasa na baadaye. “Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa na ujuzi. Mafunzo ya VETA na yale yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu yanawawezesha vijana wetu kuajiriwa au kujiajiri wenyewe, na hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwa familia zao na Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Mkuu. Katika mazungumzo ...

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Aishauri Tume ya Kurekebisha Sheria

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mheshimiwa Mayeka Mayeka, ameishauri Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kushirikiana na Halmashauri za wilaya wakati wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu maboresho ya sheria mbalimbali nchini. Akizungumza leo tarehe Agosti 6, 2025 wakati alipotembelea banda la Tume hiyo wakati wa maonesho ya Nanenane yanayoendelea viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma , Mh. Mayeka alisema ofisi za halmashauri zina mtandao mpana wa kuwafikia wananchi, hivyo zinaweza kusaidia Tume kupata maoni ya watu wengi kutoka makundi mbalimbali ya jamii. “Ni muhimu Tume ikazitumia halmashauri kama daraja la kufikia wananchi wengi, hasa walioko vijijini, ambao mara nyingi wanakosa fursa ya kutoa maoni yao kwenye mchakato huu muhimu wa kisheria,” alisema Mh. Mayeka. Mhe.Mayeka aliongeza kuwa Sheria bora ni zile zinazotokana na ushirikishwaji wa wananchi kwa kiwango kikubwa, kwani zinakuwa zimezingatia changamoto, maoni na mahitaji halisi ya jamii. Kwa upande wake Bi. Vicky Mbunde amb...

Uhuru Kenyata;Nitaunga Mkono Raila Odinga Kuwania Urais ikiwa ataachana na Rais Ruto

  CHAMA cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta kimetangaza kuwa kiko tayari kumuunga mkono Kinara wa ODM Raila Odinga kuwania urais 2027 kikisema kuwa bado kinamtambua kama Kiongozi wa Muungano wa Azimio. Naibu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe, amesema kuwa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, jana aliwaambia kuwa yupo tayari kumuunga Raila mnamo 2027 mradi tu asambaratishe uhusiano wake na utawala wa sasa. Bw Kenyatta jana aliongoza mkutano wa Kamati Kuu ya Jubilee kwenye makao makuu ya chama hicho, kikao kilichofanyika baada ya mrengo wake kushinda kesi ya mzozo wa uongozi wa Jubilee mahakamani. “Bado tunamtambua Raila kama kiongozi wa Azimio. Na kama muungano tunaamua mwelekeo wetu, hata hivyo nakuambia tuko na Tinga (Raila) hadi hali iwe vingine. Raila ndiye kiongozi wetu na Uhuru mwenyekiti wetu,” akasema Bw Murathe. “Watu pia wanaweza kuamua tuunde muungano mpya na tuwashirikishe viongozi wengine zaidi,” akaongeza. Chama cha Jubilee kinaonekana kimeshaa...

Umoja na Mshikamano ni Silaha ya Mtangamano Imara wa Sadc

Umoja na mshikamano imeelezwa kuwa ni silaha pekee ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ya kuimarisha mtangamano imara na wenye nguvu, utakaowezesha kufikia malengo yaliyowekwa na jumuiya hiyo. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kikao cha Maafisa Waandamizi wa SADC ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Zimbabwe, Balozi Albert Chimbindi alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi ya kikao hicho jijini Antananarivo Agosti 06, 2025. Katika kikao hicho ambacho ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban imeshuhudiwa Zimbabwe kupitia Balozi Chimbindi ikikabidhi uenyekiti wa kikao hicho kwa Madagascar ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Eric S. Ratsimbazafy alipokea na kuahidi kuendeleza yale yote mazuri yaliyoanzishwa na mtangulizi wake. Balozi Chimbindi alisema katika kipindi cha uenyekiti wake, mtangamano wa SADC umeendelea kuimarika na mafanikio makubwa yamepa...

Mchengerwa: Miaka 10 ya mapinduzi ya fikra, naomba ridhaa tuijenge Rufiji ya ndoto yetu

Na John Jayros  Mbunge anayetetea jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika kipindi chote amekuwa mtumishi wa watu, mwanamapinduzi wa kweli anayejali maendeleo ya wananchi hivyo amewaomba wajumbe wampe ridhaa ya kuwaongoza ili kuendelea kuleta maendeleo. Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kesho kwenye kura za maoni kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa mara ya tatu mfulizo. Mkutano huo umefanyika Ikwiriri na uliohudhuriwa na maelfu ya wajumbe na wananchi waliokuja kusikuliza sera za watia nia wanne wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na Mhe. Mchengerwa anayetetea jimbo lake. Amesema katika kipindi chake cha miaka 10 cha mapinduzi ya fikra na mageuzi makubwa ya maendeleo jimboni humo kumekuwa na mabadiliko kwenye kila sekta. "Ndugu zangu katika safari hii sote tumejionea mapinduzi na mafanikio yaliyopatikana hivyo nawaombeni kwa kasi hii hii nipeni imani ili tuendelee kufanya maendeleo ya kweli ya jimbo letu". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa  A...

Maendeleo ya Elimu ni Mkombozi wa Taifa Lolote Duniani-Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maendeleo katika sekta ya elimu ndio mkombozi na mafanikio ya Taifa lolote duniani. Amesema kwa kutambua hilo, uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliamua kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora katika ngazi zote. Amesema hayo wakati alipozungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025. “Mliopo shuleni na mnaokuja, tambueni kuwa tuna maeneo muhimu ya kuwaelimisha, mtapata elimu iliyobora na imara itakayowapa maarufa na ujuzi ili muweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi” Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho ya mitaala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo duniani ikiwemo mahitaji makubwa ya ajira kwa vijana. “Mabadiliko haya yameifanya mitaa...