Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akutana na Rais wa Afrexim bank

*_Aibua maeneo ya uwekezaji, ushirikiano zaidi na Tanzania_* WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Rais Mteule na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Biashara ya Afrika (Afreximbank), Dkt. George Elombi na kuainisha maeneo zaidi ya uwekezaji nchini Tanzania. Mheshimiwa Majaliwa amesema anaamini kuwa katika kipindi cha uongozi wa Dkt. Elombi, benki hiyo itaongeza kwa kiwango kikubwa mchango wake katika kusukuma mbele biashara, maendeleo ya viwanda na uwekezaji wa kimkakati barani Afrika ikiwemo Tanzania. “Tunapenda kukuhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kujitolea kikamilifu katika ushirikiano wake wa kimkakati na Afreximbank,” alisema. Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Majaliwa alihimiza umuhimu wa Afreximbank kukamilisha mpango wake wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha tiba nchini Tanzania (African Medical Centre of Excellence) ambacho kitakuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi na pia kupunguza utegemezi wa rufaa za nje ya...

TADB yabeba maonyesho ya nane nane kwa milioni 400

Na Mwandishi Wetu, Dodoma BENKI ya Maendeleo ya Kilimo (TADB),imemshukuru Rais Samia Sulunu Hassan kwa kuipa fedha nyingi ambazo zimeiwezesha kuwakopesha wakulima wengi na hatimaye kutangazwa kuwa mionghoni mwa benki kubwa nchini Benki hiyo ndiyo  imekuwa Mdhamini Mkuu wa maonyesho ya wakulima  ya nane nane yanayoanza kesho Ijumaa kwenye viwanja vya nane nane mkoani Dodoma ambapo Makamu wa Rais Dk Philip Mpango anatarajiwa kuyatembelea. Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege wakati akizungumza na waandishi wa habari ,kuhusu maonyesho hayo na udhamini wa milioni 400 wa benki hiyo kwenye maonyesho hayo. Alisema TADB imeamua kudhamini maonyesho  hayo kama sehemu ya shamra shamra za kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 na mafanikio makubwa waliyoyapata. Alisema TADB imefanya mambo makubwa kwenye sekta ya kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na sekta mbalimbali za serikali. Alisema benki hiyo ime...

Devotha na Samira Wang'ara Ubunge Viti Maalum Mkoa wa Kagera

 Devotha Daniel Mburarugaba na Samira Khalfani Amour wameibuka washindi kati ya wagombea nane walioshiriki katika uchaguzi wa kura za maoni nafasi ya ubunge wa viti maaluma mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa wanawake Tanzania (UWT). Akitangaza matokeo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi huo mjumbe wa baraza kuu UWT Taifa Yasmin Bachu amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na wagombea nane, jumla ya wapiga kura walikuwa 1,483 ambapo kura moja ilihalibika hivyo kura halili zikiwa 1,482. Bachu amewataja Devotha Daniel aliyepata kura 1,308 na Samira Khalfani 1,250 kuwa wameongoza katika uchaguzi huo wakifuatiwa na Anitha Korongo kura 153,Elizabeth Ngaiza kura 94,Anitha Bunono kura 52,Anitha Nyamzinga kura 44,Herieth Lugaju kura 37 na Evastina Godian kura 26. Aidha Bachu amewashauri wajumbe wa UWT mkoa wa Kagera kuwa wakati wa kampuni za Dk.Samia Suluhu Hassan wapaze sauti kwa na kuunganisha nguvu za kumuombea kura zitoshe pia kushinda majinbo yote rb ya mkoa wa Kagera ili kuwawezesha washindi hao w...

Baada ya Jina Lake Kukatwa;Alex Msama atoa neno

Siku moja tu baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuondoa jina lake miongoni mwa watia nia wa Jimbo la Ubunge Ukonga jijini Dar, aliyetia nia, Alex Msama ametoa neno zito. Msama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions & Dira Media ametoa neno kwa kuwataka watia nia wote waliokatwa majina yao nchini kote kutoa ushirikiano kwa wale ambao majina yao yanakwenda kupigiwa Kura za Maoni ngazi ya kata na hatimaye kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025. Huyu hapa Alex Msama: "Nilitia nia kuomba kuteuliwa na chama changu kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Lakini isivyo bahati jina langu halikurudi. "Siyo kwamba sifai. Nafaa ila jina langu halikurudi. Kwa wakati huu wamepatikana wengine ambao wamepewa nafasi na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama chetu ili kuendelea na mchakato. "Sisi sote ni wana CCM. Kwa hiyo wote tuna sifa ila waliopitishwa wanafaa kwa sasa. Nawaomba watia nia we...

Waziri Mkuu Ahimiza Mahusiano ya Kidiplomasia na Kibiashara Kati ya Tanzania na Grenada

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Grenada, Dickon Thomas Mitchell na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza mahusiano kidiplomasia na kibiashara kwa manufaa ya pande zote mbili. Amesema kuwa Tanzania itaendelea kutumia Jukwaa la Nne la Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (ACTIF2025) kama daraja la kukuza ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele yakiwemo kilimo, uvuvi, afya na elimu ili kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili. Katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa mwenyeji wake jijini St. George’s, Grenada, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Grenada na kubadilishana uzoefu katika teknolojia na maarifa ya kitaalamu hususan katika sekta za uzalishaji na huduma ili kuimarisha uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa vijana. Kwa upande wake, Mheshimiwa Mitchell alisema kuwa malengo ya nchi hiyo kupitia jukwaa la ACTIF ni kuhakikisha kuwa nchi za Karibiani na Afrika, zikiwemo Tanzania na Grenada...

Salum Kinyoro Ateuliwa Kura za Maoni Ccm Ubunge Jimbo la Handeni Mjini

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha mfanyabiasha maarufu Salum Kinyoro 'Kibakuli' kupigiwa kura za maoni za ubunge wa Jimbo la Handeni mjini. Salum atachuana na wagombea wengine watano. Katibu wa Itikadi na Uenezi, Amos Makala ametangaza majina hayo leo Julai 29, 2025.