Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Devotha na Samira Wang'ara Ubunge Viti Maalum Mkoa wa Kagera

 Devotha Daniel Mburarugaba na Samira Khalfani Amour wameibuka washindi kati ya wagombea nane walioshiriki katika uchaguzi wa kura za maoni nafasi ya ubunge wa viti maaluma mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa wanawake Tanzania (UWT). Akitangaza matokeo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi huo mjumbe wa baraza kuu UWT Taifa Yasmin Bachu amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na wagombea nane, jumla ya wapiga kura walikuwa 1,483 ambapo kura moja ilihalibika hivyo kura halili zikiwa 1,482. Bachu amewataja Devotha Daniel aliyepata kura 1,308 na Samira Khalfani 1,250 kuwa wameongoza katika uchaguzi huo wakifuatiwa na Anitha Korongo kura 153,Elizabeth Ngaiza kura 94,Anitha Bunono kura 52,Anitha Nyamzinga kura 44,Herieth Lugaju kura 37 na Evastina Godian kura 26. Aidha Bachu amewashauri wajumbe wa UWT mkoa wa Kagera kuwa wakati wa kampuni za Dk.Samia Suluhu Hassan wapaze sauti kwa na kuunganisha nguvu za kumuombea kura zitoshe pia kushinda majinbo yote rb ya mkoa wa Kagera ili kuwawezesha washindi hao w...

Baada ya Jina Lake Kukatwa;Alex Msama atoa neno

Siku moja tu baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuondoa jina lake miongoni mwa watia nia wa Jimbo la Ubunge Ukonga jijini Dar, aliyetia nia, Alex Msama ametoa neno zito. Msama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions & Dira Media ametoa neno kwa kuwataka watia nia wote waliokatwa majina yao nchini kote kutoa ushirikiano kwa wale ambao majina yao yanakwenda kupigiwa Kura za Maoni ngazi ya kata na hatimaye kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025. Huyu hapa Alex Msama: "Nilitia nia kuomba kuteuliwa na chama changu kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Lakini isivyo bahati jina langu halikurudi. "Siyo kwamba sifai. Nafaa ila jina langu halikurudi. Kwa wakati huu wamepatikana wengine ambao wamepewa nafasi na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama chetu ili kuendelea na mchakato. "Sisi sote ni wana CCM. Kwa hiyo wote tuna sifa ila waliopitishwa wanafaa kwa sasa. Nawaomba watia nia we...

Waziri Mkuu Ahimiza Mahusiano ya Kidiplomasia na Kibiashara Kati ya Tanzania na Grenada

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Grenada, Dickon Thomas Mitchell na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza mahusiano kidiplomasia na kibiashara kwa manufaa ya pande zote mbili. Amesema kuwa Tanzania itaendelea kutumia Jukwaa la Nne la Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (ACTIF2025) kama daraja la kukuza ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele yakiwemo kilimo, uvuvi, afya na elimu ili kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili. Katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa mwenyeji wake jijini St. George’s, Grenada, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Grenada na kubadilishana uzoefu katika teknolojia na maarifa ya kitaalamu hususan katika sekta za uzalishaji na huduma ili kuimarisha uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa vijana. Kwa upande wake, Mheshimiwa Mitchell alisema kuwa malengo ya nchi hiyo kupitia jukwaa la ACTIF ni kuhakikisha kuwa nchi za Karibiani na Afrika, zikiwemo Tanzania na Grenada...

Salum Kinyoro Ateuliwa Kura za Maoni Ccm Ubunge Jimbo la Handeni Mjini

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha mfanyabiasha maarufu Salum Kinyoro 'Kibakuli' kupigiwa kura za maoni za ubunge wa Jimbo la Handeni mjini. Salum atachuana na wagombea wengine watano. Katibu wa Itikadi na Uenezi, Amos Makala ametangaza majina hayo leo Julai 29, 2025.

Majaliwa: Actif 2025 itoe Majibu ya Changamoto za Kibiashara na Uwekezaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Jukwaa la Nne la Biashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (ACTIF) linapaswa kuja na majibu ya changamoto za kibiashara na uwekezaji zinazoyakabili mataifa ya Afrika na yale ya eneo la Karibiani. Amesema kuwa changamoto hizo zinapaswa kujadiliwa kwa uwazi na kutaja bayana vikwazo vyote vinavyosababisha kutofanyika kwa biashara kati ya mataifa hayo Ameyasema hayo jana (Jumatatu, Julai 28, 2025) wakati akishiriki mjadala ya Wakuu wa Nchi na Serikali kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Nne la Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (Afri-Caribbean Trade and Investment Forum-ACTIF 2025) linalofanyika katika kituo cha mikutano cha Radisson jijini St. George’s, nchini Grenada. Mheshimiwa Majaliwa anahudhuria jukwaa hilo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Mbali ya kujadili changamoto hizo, nchi zetu zinapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye mataifa...

Kampeni ya "Badilika, Tokomeza Ukatili"

  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amezindua rasmi kampeni ya 'Badilika, Tokomeza Ukatili' itakayotekelezwa kwa miaka miwili 2025/27 mkoani Kigoma. Akizindua kampeni hiyo iliyoandaliwa na shirika la maendeleo la nchini Ubelgini ENABEL katika uwanja wa Mwanga Centre mkoani Kigoma Jumatatu Julai 28, 2025, Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito kwa jamii kubadili tabia, mitazamo na mienendo inayochochea ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Amesisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko huku akijiunga mwenyewe kama balozi wa mabadiliko na Kampeni ikilenga kuvuna mabalozi 150,000 katika mkoa huo. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msukumo mkubwa katika kutokomeza ukatili kupitia sera madhubuti na mikakati ya kitaifa kama Sera ya Taifa ya Jinsia ya mwaka 2023 na Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II). Aidha Waziri Dkt. Gwajima ameli...