Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MAGEREZA YAIPIGISHA KWATA POLISI BAMMATA 2026

 Na Ssgt Mawazo Mtondo – MWANZA Timu ya mpira wa pete ya Jeshi la Magereza imeendeleza kiwango chake kizuri katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 63–36 dhidi ya timu ya Polisi Tanzania katika mchezo uliochezwa leo, Septemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, timu ya Magereza ilionyesha uwezo mzuri katika kujenga mashambulizi na kutumia vyema nafasi ilizopata, hali iliyoiwezesha kufunga magoli 63 na kuibuka na ushindi wa kishindo dhidi ya Polisi. Ushindi huo unaendeleza mwendelezo mzuri wa Kanda ya Magereza katika mashindano hayo, baada ya awali kuifunga Kanda ya JKT Tanzania kwa magoli 46–43.

NMB YARUHUSU VIFAA VYA UCHIMBAJI KUTUMIKA KAMA DHAMANA YA MKOPO

   Benki ya NMB imeweka utaratibu unaowawezesha wachimbaji wadogo kutumia vifaa vya uchimbaji kama dhamana ya kupata mkopo, hatua inayolenga kupunguza changamoto ya dhamana inayowakabili wachimbaji wengi. Akizungumza katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Mkuu wa Idara ya Biashara NMB, Deogratias Shirima, amesema kupitia utaratibu huo mchimbaji anaweza kupata kati ya asilimia 50 hadi 80 ya thamani ya vifaa anavyohitaji kulingana na tathmini na vigezo vya benki. Amesema jumla ya zaidi ya Sh bilioni 350 zimetolewa na benki hiyo hadi kufikia Julai mwaka huu kwa ajili ya shughuli zinazohusiana na sekta ya madini, huku fedha hizo zikiwanufaisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini, wakiwemo wachimbaji wadogo, kampuni pamoja na watoa huduma. Amesema NMB imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo kupata mitaji kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu, pamoja na elimu ya fedha, mazingira na matumizi bora ya ardhi kwa kushirikiana ...

TPDC YANG’ARA MAONESHO YA TISA YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limejitokeza kwa kishindo katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu fursa na teknolojia zinazotumika katika sekta ya mafuta na gesi nchini. Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Masoko wa TPDC, Grace Chigugu, amesema ushiriki wa TPDC unalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu majukumu ya shirika hilo, pamoja na fursa zinazopatikana katika sekta ya mafuta na gesi asilia. Grace amesema TPDC inatekeleza majukumu yake ya kimkakati kuanzia katika utafiti na utafutaji wa mafuta na gesi, uzalishaji, uchakataji hadi usambazaji wa nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali. Ameeleza kuwa katika maonesho hayo, wataalamu wa TPDC wanatoa elimu kuhusu matumizi ya teknolojia za kisasa zinazosaidia katika utambuzi wa miamba yenye viashiria vya mafuta na gesi, pamoja na mifumo ya kisasa ya uchorongaji na usafirishaji. Aidh...

AZANIA BANK YAWEKA MKAKATI MPYA WA KUONGEZA TIJA SEKTA YA MADINI

  Na Wellu Mtaki, Geita Benki ya Azania imeweka mkakati wa kuimarisha na kuongeza tija katika sekta ya madini nchini kwa kuwawezesha wadau mbalimbali wa sekta hiyo kupata mikopo yenye masharti rafiki, inayolenga kukidhi mahitaji ya kifedha katika hatua tofauti za mnyororo wa thamani wa madini, kuanzia wachimbaji wadogo hadi wawekezaji wakubwa. Kwa mujibu wa benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Tisa ya Madini Geita, imeeleza kuwa inatoa mikopo ya mitaji inayolipwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya kuendesha na kukuza biashara. Pia, benki hiyo inatoa mikopo ya uwekezaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayohusiana na shughuli za uzalishaji. Mbali na mikopo hiyo, Benki ya Azania inatoa pia mikopo kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na vifaa vya uzalishaji, ikiwemo mashine mbalimbali za viwandani pamoja na vifaa vinavyoweza kutumika katika shughuli za kutengeneza bidhaa kama betri. Aidha, benki hiyo imeeleza kuwa inawezesha wadau wa sekta ya madini kupata mik...

CHACHA YUPO SAHIHI: CCM NDIO MMILIKI WA JWTZ, POLISI NA USALAMA - HATA UPINZANI UKICHUKUA NCHI UTAFANYA HIVYO

Na Mwandishi Wetu Kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Ndugu Paul Chacha, kuwa CCM ndio wamiliki wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa na kwamba vyombo vyote vya dola ni mali ya CCM,  imezua mjadala mkubwa nchini.  Hata hivyo, wachambuzi wa sayansi ya siasa, historia na itikadi wamemuunga mkono na kusema Chacha amesema ukweli mtupu wa kisayansi na uhalisia wa madaraka ambao watu wengi wanaogopa kuusema hadharani. Dkt Johnson Willium, Mchambuzi wa Siasa za Ulinganishi na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu Cha Makerere Uganda, anasema Chacha yupo sahihi kwa asilimia mia moja na ametoboa siri ya miaka hamsini.  Dkt Willium anasema, "Duniani kote kuanzia Marekani, Urusi, China na hata nchi za Afrika, jeshi ni mali ya chama kilichopo madarakani. Hii ni nadharia inaitwa State-Party Fusion. Marekani jeshi lake linamilikiwa na Republican au Democrat aliyepo Ikulu. Urusi linamilikiwa na Un...

POLITICAL ANALYSTS AGREE: COMRADE CHACHA TELLS THE TRUTH ABOUT PARTY AND STATE

  BY Staff Writer Dar es Salaam - Political analysts have unanimously agreed and vindicated the Secretary of the National Executive Council of CCM for Organization, Comrade Paul Chacha, for his bold and truthful statement that CCM is the owner of the TPDF, Police and National Security, saying Chacha has spoken the scientific truth about the fusion of party and state that many fear to say in public. According to analysts, Chacha is 100 percent correct, and even any opposition party that takes over the country will do the same and even more. The debate that has divided social media for days has now been settled by experts. Speaking from different universities and political schools, analysts say Chacha did not make a mistake, he taught a political science class on how power works in Tanzania and the world. They say what Chacha said is not just politics, it is the reality of state power. Dr. Johnson Willium, an Analyst of Comparative Politics and International Relations from Makerere U...