Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.
Chemba ya Taifa ya biashara (TNCC) yamtunuku tuzo maalum waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Lameck Nchemba kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha mazingira ya biashara, uwekezaji na kukuza ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi hapa nchini.
Tuzo imetolewa katika hafla iliyowakutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo, ambapo TNCC imeweza kueleza kuwa hatua hiyo inalenga kutambua watu na taasisi zilizochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Rais wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC), Bw. Vicent Minja amemwambia Waziri Mkuu kuwa tuzo hii ni ishara ya kutambua mchango wako mkubwa katika kuimarisha mazingira ya biashara nchini.
" Uongozi wako umefungua milango ya ushirikiano imara kati ya serikali na sekta binafsi, jambo ambalo limeongeza imani ya wawekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini", amesema Minja
Viongozi na wadau wengine pia wameweza kupata tuzo kwa waliotambuliwa kwa mchango wao katika sekta binafsi na maendeleo ya uchumi.
Miongoni mwa waliotunukiwa ni Bi. Emma Kawawa, ametambuliwa kwa mchango wake katika kuendeleza ujasiriamali wa wanawake na uongozi katika biashara akiwemo Bw. David Mwaibula kwa mchango wake katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Bwana Imani Kajula, Bw. Elibariki Mmasi na Bi. Mercy, ambao wametambuliwa kwa mchango wao katika kukuza ubunifu, uongozi na maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi na kutunukiwa tuzo hizo.
Pia Mfanyabiashara mashuhuri na Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Azizi, naye ametunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya biashara, uwekezaji na kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
TNCC imeeleza kuwa utoaji wa tuzo hizo ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha ubora, uwajibikaji na mchango chanya katika sekta ya biashara.
TNCC inasisitiza kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi endelevu.













Comments
Post a Comment