RC ARUSHA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI HOYCE TEMU WAKATI TANZANIA IKIJIANDAA NA MKUTANO WA 153 WA BUNGE LA DUNIA
Na Prosper Makene
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Alhamisi Septemba 24, 2026 Ofisini kwake Jijini Arusha, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa- Geneva Uswisi, Balozi Dkt. Hoyce Anderson Temu.
Balozi Temu yupo Mkoani Arusha kushirikiana na Serikali katika maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Bunge la dunia (IPU), utakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 hadi 09, Oktoba mwaka huu, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa mkutano huu mkubwa wa kihistoria utakaowakutanisha Maspika na Wabunge kutoka Nchi 183 wanachama wa IPU, Mkutano ukiwa na kaulimbiu isemayo "Kuimarisha utawala bora na kuwezesha jamii kupitia ushirikishwaji, imani na fursa kwa wote."



Comments
Post a Comment