Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JWTZ KUKAMILISHA HOSPITALI YENYE HADHI SAWA NA MUHIMBILI

 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liko katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa hospitali yenye hadhi sawa na Hospitali ya Taifa Muhimbili inayojengwa katika eneo la Msalato, jijini Dodoma. Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakati kamati hiyo ilipotembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa afya. Luteni Jenerali Othman amesema hospitali hiyo itakuwa na miundombinu ya kisasa pamoja na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, hatua ambayo itasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na wananchi kwa ujumla. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU),Mheshimiwa  Paschal Inyasi Chinyele, amepongeza maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo na kueleza kuwa mradi huo ni muhimu kwa kuimarisha hud...

RAIS SAMIA ANAYAJALI MAKUNDI MAALUM, AMEONGEZA MIKOPO KUTOKA ASILIMIA 10 HADI 15 - CHATANDA

 NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum sasa wamefikiwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, kufuatia bajeti hiyo kuongeza asilimia za mikopo ya makundi hayo kutoka asilimia kumi hadi 15. Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mary Chatanda, Juni 23, 2026, Jijini Dodoma, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayajali makundi hayo kwa maneno na kwa matendo, ndiyo maana ameamua kuongeza asilimia za mikopo yao. "Uwezeshaji wananchi kiuchumi hasa makundi ya wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum ni miongoni mwa vipaumbele vya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameona asilimia kumi haitoshi, ameongeza asilimia tano zaidi ili kuhakikisha makundi hayo yananufaika na fursa za kiuchumi kwa ustawi wao," amesema Chatanda. Sambamba na hilo, Chatanda amesema katika mipango ya maendeleo ni vyema kuhakikisha makund...

UJUMBE WA NAMIBIA WAVUTIWA NA KAIRUKI GREEN IVF

 Na Mwandishi Wetu UJUMBE kutoka Wizara ya Afya ya Namibia pamoja na wafanyabiashara walioambatana na Rais wa Namibia katika ziara yake ya hivi karibuni umetembelea Hospitali ya Kairuki na kujionea maendeleo ya huduma za afya, elimu ya tiba na uzalishaji wa dawa zinazotolewa na taasisi hiyo. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mganga Mkuu  wa Hospitali ya Kairuki, Dk, Sia Kiwia, alisema wageni hao walipata fursa ya kutembelea idara mbalimbali na kujifunza teknolojia za kisasa zinazotumika katika utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania. Alisema moja ya maeneo yaliyowavutia zaidi ni huduma ya matibabu kwa kutumia teknolojia ya HIFU (High-Intensity Focused Ultrasound), mtambo unaowezesha kuondoa uvimbe bila kufanyika upasuaji. “Wameweza kuona mtambo wetu wa HIFU unaotibu uvimbe mbalimbali kwenye matiti, ini, kongosho, kizazi na tezi dume kwa wanaume Pia wamejionea aina za wagonjwa wanaoweza kufaidika na teknolojia hii na mchango wake katika kuboresha huduma za afya,” alisema  ...

TANZANIA, MEXICO DEEPEN DIPLOMATIC TIES IN GENEVA MEETING

 By Prosper Makene *GENEVA, 2026* — Bilateral engagement between Tanzania and Mexico continued this week as Dr. Hoyce Temu, Tanzania’s Deputy Permanent Representative in Geneva, met with Ambassador Fernando Israel Espinosa Olivera, Mexico’s Deputy Permanent Representative, for a courtesy call at the Mexico Mission. “Strengthening Tanzania-Mexico relations means finding practical intersections where our priorities meet global challenges,” Dr. Temu said. The dialogue centered on building shared vocabulary to support future cooperation, with terms like “shared stewardship” and “community-led data” emerging as common ground. “Courtesy calls don’t produce signatures,” Dr. Temu added. “They produce the trust and terminology that make later agreements possible.” Dr. Temu later noted the discussion in a brief statement: “Courtesy to the Mexico Mission in Geneva. Great discussions with the deputy permanent representative on many fronts related to bilateral diplomacy.” Tanzania and Mexico es...

DPP KENYA;WANAFUNZI SITA KUKABILIWA NA MASHTAKA 16 YA MAUAJI

  Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) nchini Kenya imeidhinisha kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya wanafunzi Sita wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la moto lililotokea katika shule ya Utumishi Girls Academy, Kaunti ya Nakuru, tarehe 28 Mei 2026. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisi ya DPP tarehe 23 Juni 2026, faili la uchunguzi wa awali lililowasilishwa na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) limefanyiwa tathmini ya kina na kubaini kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuendelea na hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa. DPP amesema kuwa wanafunzi wanaohusishwa na tukio hilo watakabiliwa na mashtaka 16 ya mauaji, yakitokana na vifo vya wanafunzi 16 vilivyoripotiwa kufuatia ajali hiyo ya moto iliyotikisa taifa la Kenya. Katika taarifa hiyo, DPP ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la matukio ya uchomaji moto na vitendo vingine vya uhalifu vinavyoripotiwa katika taasisi za elimu nchini humo. Aidha, amesisitiza kuwa watu wote watakaobainika kuhusika na makosa...

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YACHANGIA VIFO VINGI NCHINI-MCHENGERWA

 Waziri wa Afya, Mhe Mohammed Mchengerwa amesema kuwa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza yamesababisha vifo kwa watoto wachanga kuanzia umri wa mwaka 1 hadi 5 zaidi ya elfu 12 kila mwaka huku ugonjwa wa kansa ukikatisha maisha ya watanzania zaidi ya elfu 43 kila mwaka. Hayo amebainisha leo Juni 23, 2026 jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa Kimataifa wa Kimkakati wa Kikanda wa PEN-Plus (ICPPA 2026), unaowakutanisha viongozi, watunga sera, wataalamu wa afya, watafiti, washirika wa maendeleo na wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika na sehemu nyingine za dunia ambapo amesema magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza huchukua zaidi ya asilimia 20 kila mwaka katika mfuko wa bima wa NHIF. Aidha, Waziri Mchengerwa amesema kuwa serikali imejipanga katika kujikinga na magonjwa hayo yasiyokuwa ya kuambukiza huku akimpongeza Rais Samia kwa kufanikisha kupeleka vifaa tiba mbalimbali katika vituo vya afya ili kusaidia kuwafikishia huduma bora ya afya wananchi. Kwa upande wake mkur...