Na Jovina Massano Musoma.
Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Musoma mkoani Mara yahamasisha mashirika yasiyo ya kiserikali ( NGO) kuelimisha jamii dhidi ya tahadhali ya mvua za el nino kama ilivyotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini.
Hayo yamesemwa wakati wa kongamano la Mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali lililohisisha mashirika zaidi ya 50 yaliyopo katika Manispaa hiyo.
Kongamano hilo lenye lengo la kujenga fikra mpya katika upatikanaji wa rasilimali fedha kupitia vyanzo vya ndani limeweza kufanya majadiliano mbalimbali yanayohusu jamii ikiwemo uwasilishaji wa taarifa kwa NGO za mwaka 2025/2026.
Aidha mashirika yametakiwa kushirikiana na kuhakikisha yanaboresha taarifa zao kupitia mfumo uliopo kuwezesha taarifa kupatikana kwa urahisi ikiwemo uwasilishaji.
Akitoa hamasa hiyo Loserian Mollel Saning'o afisa mradi kutoka shirika la Victory Hope Foundation Tanzania (VIHOFOTA) kwa niaba ya Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa hiyo amesema mashirika yashiriki kikamilifu katika uelimishaji wa tahadhali ya mvua hizo.
Amesisitiza kuwa kinga ni bora kuliko tiba uchukuaji hatua za mapema na tahadhali kwa jamii ni salama zaidi.
Amezikumbusha jamii kutunza nyaraka muhimu mfano vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya taaluma kwa kuweka katika nailoni au eneo ambalo endapo changamoto ikijitokeza vitaendelea kubaki salama.
Baadhi ya viongozi wa NGO wameshauri mashirika kuwa na ubunifu wa kuandaa maandiko ya miradi yenye tija na kuweza kupata ufadhili kwa wakati pia kutoa huduma bora kwa walengwa kwa kuwa na kiasi Cha huduma ili kuifanya bora zaidi yenye matokeo chanja.
Nae Jovina Massano Katibu mtendaji wa Amani na Maendeleo Organization ( AMO) amewazitaka mamlaka zinazotoa huduma kwa NGO hasa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) kutoa huduma kwa wakati ili NGO zinazoanza kuanza kutoa huduma tarajiwa kwa wakati.
"Kumekuwa na changamoto za kuchelewesha utambulisho kutoka TAMISEMI licha ya kuwa tayari Shirika limekwisha sajiliwa na kupata cheti cha usajili hii inachangia shirika kushindwa kuanza shughuli kwa wakati ilihali kuna uwepo wa utoaji wa taarifa kwa Wizara husika ni vema utambulisho utolewe kwa wakati", amesema Jovina.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Musoma Jacqueline Wanzagi amezitaka NGO kushiriki kikamilifu katika uelimishaji wa tahadhali ya mvua tarajiwa za el nino na kushiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.
Pia wamezitaka NGO kuwa sehemu ya washiriki kwa kutoa huduma kwa wahanga endapo janga litatokea na kujihusisha jirani na jamii kwa kusaidia kwa karibu.
Miongoni mwa maafisa wa Idara hiyo waliokuwepo ni Juma Njwayo na Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Octavian Rweyemamu ambae amesisitiza NGO kutumia mfumo kuwasilisha taarifa zao kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
NGO zimeazimia kushiriki kikamilifu katika uelimishaji na utoaji huduma za majanga katika kipindi cha mvua na wapo tayari kuanza kusafisha maeneo mbalimbali hasa yaliyo kwenye hatari ya kuathiriwa.
Miongoni mwa mashirika yaliyoshiriki ni pamoja na Powerlife,Victory Hope Foundation Tanzania (VIHOFOTA),Amani na Maendeleo Organization (AMO),
Rising Hope Organization Tanzania,MWEA,Jipe moyo Center, Watoto Wapinge Ukimwi,TACCO,UTU Foundation Tanzania,Haki Sawa,ICCAO na MACCO.
Aidha Wananchi wamekumbushwa kuwa na vifaa vya dharura kamaTochi , dawa muhimu namba za simu za viongozi wa Serikali za mitaa lengo ikiwa kama kuna changamoto ya maafa taarifa ifike kwa Mwenyekiti kwani itawezesha msaada wa haraka pindi janga linapokuwa limetokea.
Kauli mbiu ya kongamano inasema "Fikra mpya kuhusu uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali,ubunifu,ubia na upatikanaji wa rasilimali fedha kupitia vyanzo vya ndani",







Comments
Post a Comment