Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini amewataka Wananchi wa Mkoa wa Mbeya hasa Wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi stahiki kwa mjibu wa Sheria ikiwemo kutoa risiti na unapotoa huduma na kudai risiti baada ya kununua ili kuendelea kuchochea uchumi utakaosaidia kujenga na kuboresha miradi ya Maendeleo ndani ya Mkoa wa Mbeya.
Mhe. Sagini amesema Miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani Mbeya inategemea Uwepo wa Uchumi na ni Makusudio mema ya Serikali kuhakikisha uchumi unaimarika katika viwango vya Nchi na hata Uchumi wa Mtu mmoja mmoja na viwango vyote vinategemea ukusanyaji Mapato.
Ameyasema hayo leo wakati wa hotuba yake ya Ufunguzi katika kikao cha Ujirani mwema kati ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Malawi yaliyoketi kwa lengo ya kujadili hali ya Usalama na uimarishwaji wa Amani kati ya Nchi hizi hususani kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini inayopakana na Nchi ya Malawi.
Aidha Mhe. Sagini amewaomba wananchi Kuchukua tahadhari dhidi ya Mvua za El- nino zinazotarajiwa kunyesha kuanzia Mwezi Septemba 2026 hadi mwanzoni mwa Mwaka 2027 na kuwasisitiza kujiepusha na Vitendo au Mazingira yanayoweza kuchochea hali ya utosefu wa Usalama na Amani hususa ni kwa wale wanaoishi Mipakani.
Kwa Miaka kadhaa sasa umekuwa ni utaratibu wa Majeshi ya Tanzania Wakiongozwa kwa Sasa na Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myala kutoka Brigedi ya Kusini kukutana na kufanya mazungumzo na Majeshi ya Nchi zinazopakana na ukanda huu ikiwemo Malawi chini ya Brigedia Colonel MB Chimbayo Msumbiji na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) Lengo ikiwa ni kudumisha Ujirani Mwema ikiwemo uimarishwaji wa Usalama kati ya nchi hizi mbili.
Majeshi yaliyokutana leo ni Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Idara ya Usalama na Mamlaka ya Mapato kutoka nchi zote mbili yaani Tanzania na Malawi.


















Comments
Post a Comment