TANZANIA YAPIGA HATUA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO, KUWANIA KITI BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA (UN), YASUKUMA MBELE AJENDA YA AFRIKA
Tanzania imetangaza azma yake ya kuwania nafasi ya uanachama usio wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha 2029–2030, huku ikiahidi kupeleka katika chombo hicho sauti imara ya Afrika na kusukuma mbele diplomasia ya kuzuia migogoro, utatuzi wa migogoro kwa njia za amani na mageuzi ya operesheni za kulinda amani. Msimamo huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mjadala wa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unaofanyika jijini New York, Marekani. Mhe. Ndejembi amesema Tanzania ikichaguliwa itatoa kipaumbele kwa diplomasia ya kuzuia migogoro kabla haijawa vita, utatuzi wa migogoro kwa njia za amani, kuimarisha nafasi ya wanawake katika ulinzi na ujenzi wa amani, kuongeza ushiriki wa vijana katika ajenda za amani na usalama, pamoja na kusukuma mbele mageuzi ya operesheni za Umoja wa Mataifa za kulin...