Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MHANDISI SWEDI: NANENANE NI FURSA YA KUIMARISHA SEKTA YA MADINI

 DODOMA Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Aziza Swedi, amesema Maonesho ya Nanenane ni jukwaa muhimu la kuwaelimisha wananchi kuhusu Sekta ya Madini, kusikiliza maoni yao na kupata mrejesho unaosaidia kuboresha huduma na kuongeza thamani ya sekta hiyo. Mhandisi Swedi amesema hayo baada ya kutembelea mabanda ya Taasisi za Wizara ya Madini katika kilele cha Maonesho ya Nanenane jijini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika maendeleo ya sekta hiyo. Amesema maonesho hayo yanawezesha Tume ya Madini kuwafikia wananchi moja kwa moja, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kupata maoni ambayo yanaweza kutumika kuboresha utendaji na utoaji wa huduma. “Kila swali na hoja inayotolewa na mwananchi ni muhimu, kwa sababu inatusaidia kutambua maeneo yanayohitaji maboresho na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma,” amesema Mhandisi Swedi. Aidha, amesema ushiriki wa wananchi katika Maonesho ya Nanenane unaimarisha ushirikiano kati ya Serikali, taasisi zina...

MULEBA: UJENZI WA KITUO CHA KUSUKUMA MAFUTA EACOP WAFIKIA 88%

   Na Angela Sebastian ;Muleba Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi namba Tatu (PS3) kinachojengwa katika Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, kimefikia asilimia 88 ya ujenzi na kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Agosti au mwanzoni mwa Septemba mwaka huu. Kituo hicho ni sehemu ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), unaounganisha maeneo ya uzalishaji mafuta nchini Uganda na Tanzania. Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, amesema kukamilika kwa asilimia 88 ya ujenzi wa PS3 ni hatua kubwa katika utekelezaji wa mradi huo. Moshi amesema ziara ya wabia na wadau wa mradi huo katika kituo hicho imelenga kujionea maendeleo ya ujenzi na hatua zilizofikiwa pia kuweka msisitizo wa kuhakikisha vituo vyote vya kusukuma mafuta vya mradi huo vikikamilika ifikapo Desemba mwaka hatua itakayosaidia katika kukamilisha maandalizi ya uendeshaj...

TRA NA WYFI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUWA KINARA WA NISHATI SAFI AFRIKA

 NA: MWANDISHI WETU Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Women and Youth Future Initiative (WYFI) wamepongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Kinara wa Nishati Safi Barani Afrika. Pongezi hizo zimetolewa Agosti 7, 2026, Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya WYFI. Taasisi ya WYFI inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Baraka, ambapo imejikita kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi kupitia fursa mbalimbali za maendeleo.  "Kutokana na jitihada alizoonyesha Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan katika kupigania matumizi ya nishati safi ya kupikia, tumeona tumpongeze na kumtia moyo kwa kazi kubwa na nzuri anazofanya," amesema Baraka. Katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Nolasco Mlay, alimwakilisha Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mlay aliwahimiza vijana na wanawake kutokuwa tegemezi wa ajira pekee, bali kutumia ubunifu, teknolojia na mitandao ya kij...

CHONGOLO AITAKA NIRC KUKAMILISHA UGAWAJI WA PAMPU KABLA YA AGOSTI 30

 📍Nzuguni : Dodoma Waziri wa Kilimo, Mh.Daniel Chongolo, ameipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na kuitaka kuhakikisha pampu za Umwagiliaji  zilizotengwa kwa ajili ya wakulima zinagaiwa kuanzia Agosti 30 kwa wanufaika katika mikoa husika ili ziweze kutumika kuongeza uzalishaji wa mazao. Mheshimiwa Chongolo ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya John Malechela, Nzuguni, mkoani Dodoma. Amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika upatikanaji wa teknolojia za Umwagiliaji kwa lengo la kuongeza tija ya uzalishaji, hivyo ni muhimu vifaa hivyo viwafikie wakulima kwa wakati ili viweze kutoa matokeo yaliyokusudiwa. Waziri Chongolo amepongeza jitihada za Tume katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa programu mbalimbali za Umwagiliaji nchini, zikiwemo usambazaji wa pampu na utekelezaji wa miradi ya Umwagiliaji  inayolenga kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa ufan...

KAMBARAGE WASIRA AIKABIDHI BUNDA KOMPYUTA 10 ILI KUONGEZA UJUZI WA TEHAMA SHULENI

 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe.Kambarage Masato Wasira, ametoa Kompyuta 10 za Kisasa kwa ajili ya kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza matumizi ya teknolojia katika shule zilizopo katika Kata 10 za Halmashauri ya Mji wa Bunda. Kompyuta hizo zimekabidhiwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kupitia mwakilishi wa Mbunge huyo, Elly Mwabe, ambaye ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango wa Mhe.Wasira wa kuendelea kushirikiana na jamii katika kuboresha elimu, hususan katika Mkoa wa Mara. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya  Bunda Mhe.Aswege Kaminyoge amesema kompyuta hizo zitakabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda ili wataalamu na viongozi wa halmashauri wabaini maeneo yenye uhitaji mkubwa na kuzisambaza kwa shule husika. Amesema dunia ya sasa inahitaji wanafunzi kuwa na uelewa wa teknolojia, hivyo upatikanaji wa kompyuta mashuleni ni muhimu katika kuwaandaa wanafunzi kukabiliana na mahitaji ya elimu ya kisasa. “Wato...

RC SENDIGA AHIMIZA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHO YA NANENANE, KUJIFUNZA TEKNOLOJIA MPYA ZA KILIMO

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Agosti 7, 2026, akiwa mgeni rasmi wa zamu, ametembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Themi-Njiro, jijini Arusha. Katika ziara hiyo, Mhe. Sendiga ametoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo ili kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa za kilimo, mifugo na uvuvi zitakazochochea ongezeko la uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi. Amesema maonesho hayo yamekusanya wafanyabiashara, wabunifu na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi, jambo linalotoa fursa kwa wananchi kupata maarifa, kujifunza ubunifu na kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Maonesho ya Nanenane ya mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: "Tambua Soko, Ongeza Tija kwa Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050."