Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS SAMIA AIPA TADB NGUVU,MTAJI WAPAA HADI BILLIONI 452.16

 Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha sekta ya kilimo zimeendelea kuzaa matunda baada ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuongeza mtaji wake kutoka Shilingi bilioni 60 hadi kufikia Shilingi bilioni 452.16, hatua inayoongeza uwezo wa benki hiyo kufadhili kilimo, mifugo na uvuvi kwa kiwango kikubwa zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari  MAELEZO jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania TADB, Frank Nyabundege, amesema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali pamoja na ushirikiano na taasisi mbalimbali za maendeleo. Amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa TADB ulikuwa Shilingi bilioni 60 pekee, lakini sasa umefikia Shilingi bilioni 452.16, jambo linaloifanya benki hiyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi nchini. "Kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaj...

MKURUGENZI MKUU WA REA AZUNGUMZA NA WADAU KATIKA KUWEKA MIKAKATI YA USAMBAZAJI WA NISHATI YA UMEME VIJIJINI

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy leo Julai 30, 2026 amezungumza na Wajumbe wa Rural Energy Working Group, ambalo ni Jukwaa lililoundwa na REA likishirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali ambao ni Wadau muhimu katika kusambaza Nishati Bora Vijijini. Mhandisi Saidy amesema kuwa Jukwaa hilo ni muhimu sana katika kuratibu, kubadilishana taarifa na kuwa na mipango ya pamoja katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya Wakala na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya nishati bora vijijini kwa wakati.  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa REA, Mhandisi Jensen Mahavile amesema kuwa kundi hilo pia ni jukwaa muhimu kwa sababu linatoa ushauri pamoja na kutoa ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazotokea wakati wa utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati bora vijijini.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA MKURUGENZI MTENDAJI MUHIMBILI WAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI KUBORESHA MFUMO WA MALIPO YA HUDUMA ZA AFYA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Dellilah Kimambo, kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha mfumo wa malipo ya huduma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi, haraka, kwa ufanisi na kuondoa malalamiko ya wananchi. Katika kikao hicho, Dkt. Magembe amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha huduma za afya, akimtaka Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha mifumo ya TEHAMA ya hospitali inaendelea kuimarishwa ili kurahisisha mchakato wa malipo ya huduma, kuongeza uwazi kwa wananchi, kupunguza usumbufu na muda wa kusubiri kwa wagonjwa, pamoja na kuondoa udanganyifu. “Mwananchi apate taarifa za malipo anayotakiwa kufanya kiganjani mwake kupitia simu ili kabla ya kulipa ajihakikishie kama malipo hayo ni sahihi au hapana”, amesema Dr Grace.  Amemwelekeza Mkurugenzi wa Muhimbili kuimarisha usimamizi wa hu...

CHATANDA SASA MLEZI WA CCM MKOA WA MARA

 NA: MWANDISHI WETU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu (MCC), Mary Chatanda, amebadilishwa mkoa wa ulezi wa kichama na sasa ni mlezi wa CCM mkoa wa Mara. Mabadiliko hayo yamefanyika Julai 29, 2026, Zanzibar, kufuatia vikao vya Chama vinavyoendelea. Kabla ya mabadiliko hayo, Chatanda alikuwa mlezi wa mikoa ya Mjini na Magharibi, Zanzibar. Akizungumzia mabadiliko hayo, Chatanda amekishukuru Chama chake kwa kuendelea kumuamini kutekeleza majukumu mbalimbali ya kichama. "Nimepokea taarifa hii ya mabadiliko ya ulezi wa Chama mkoa kwa moyo wa unyeyekevu. Nakishukuru Chama changu kwa kuniamini. Niwaombe wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla tushirikiane kuhakikisha tunasukuma mbele gurudumu la maendeleo na Chama chetu". Ameongeza kuwa "Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imepeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo mkoani Mara, ni wajibu wetu kuhakikisha fedha hizo zina...

VISIMA 67,000: NGUVU MPYA YA KUONGEZA CHAKULA NA KIPATO CHA MKULIMA

 Arusha.  Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeanza utekelezaji wa mpango wa kuchimba visima 67,000 kwa wakulima wadogo nchini, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao, kuimarisha usalama wa chakula na kufungua maelfu ya ajira kwa vijana. Akizungumza katika Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma mwaka 2026 jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, amesema mpango huo unatekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mradi wa uchimbaji wa visima kwa wakulima wadogo katika Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Mbeya mwaka 2023. «"Lengo letu ni kumkomboa mkulima mdogo kutokana na utegemezi wa mvua kwa kuhakikisha anapata maji ya uhakika kwa ajili ya uzalishaji wa mwaka mzima. Hii itachochea uzalishaji, kuongeza kipato cha wakulima na kuimarisha usalama wa chakula nchini," amesema Mndolwa.» Amesema mpango huo pia unalenga kufikisha huduma za umwagiliaji kwa wakulima walio nje ya skimu ra...

KINGOBA: UHURU WA KUTOA MAONI UENDE SAMBAMBA NA UWAJIBIKAJI

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mjumbe wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Kaimu Meneja wa Huduma za Kiswahili wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Mgaya Kingoba, amesema uhuru wa kutoa maoni una mipaka ya kisheria na kimaadili, hivyo haupaswi kutumiwa kutoa matusi, kudhalilisha wengine, kuchochea chuki au kusambaza taarifa zisizo sahihi. Kingoba amesema hayo leo, Julai 30, 2026, alipowasilisha mada kuhusu “Kuimarisha Uzalendo katika Uandishi wa Habari ili Kulinda Amani, Umoja na Mshikamano” katika siku ya pili ya mafunzo kwa watumishi wa Bongo FM, redio dada ya TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania), yaliyofanyika katika Ofisi za JAB jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 29, 2026. Amesema ukosoaji ni sehemu muhimu ya uhuru wa kujieleza, lakini unapaswa kulenga kuonesha kasoro na kuchochea maboresho badala ya kushambulia watu, kutumia lugha ya kejeli au kubomoa imani ya jamii kwa taasisi. “Mkosoaji mzalendo hafichi makosa, lakini pia hatumii matusi, kejeli au upot...

TARURA MKOA WA LINDI YAPOKEA TUZO YA UKIDHI WA SHERIA YA MANUNUZI WA UMMA

📌Tarura Yapokea Tuzo Tatu za PPRA Arusha  TARURA Mkoa wa Lindi imepata tuzo ya Ukidhi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma kufuatia ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Tuzo hiyo imetolewa katika Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma, ikiwa ni kutambua uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma pamoja na kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma. TARURA Lindi inaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yake unazingatia misingi ya utawala bora na matumizi yenye tija ya fedha za umma.

MAWAKILI WA SERIKALI WANOLEWA KUHUSU SHERIA YA FEDHA

 Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole amefungua mafunzo maalum kwa Mawakili wa Serikali nchini, yanayohusu Sheria ya Fedha (Finance Act). Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 30 Julai, 2026 Jijini Dodoma, ambapo Mawakili wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali nchini wameshiriki kwa wingi katika mafunzo hayo kwa njia ya mtandao.  Mafunzo ya Sheria ya Fedha kwa Mawakili wa Serikali, yameratibiwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, na kuendeshwa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na Wizara ya Fedha. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwandishi Mkuu wa Sheria, ameeleza kuwa Sheria ya Fedha ni mhimili mkuu wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, hivyo Mawakili wa Serikali wana mchango mkubwa katika kuchambua, kuandika, na kuhakikisha vifungu vyake vinakidhi mahitaji ya kisheria na kiuchumi.  *“Mafunzo haya yanalenga katika kuwapitisha Mawakili wa Serikali ili muweze kufahamu nafasi yenu ...

DC KYOBYA MGENI RASMI TUKIO LA KIHISTORIA "HIKE FOR A GIRL CHILD" UDZUNGWA

 KILOMBERO  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Msomi Dkt. Dunstan Kyobya anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye tukio la kihistoria la Matembezi ya Vilimani ili kupaza Sauti kwa Ajili ya Mtoto wa Kike, _"Hike for A Girl Child"_. Tukio hilo lenye lengo la kuvunja ukimya na unyanyapaa masuala ya Hedhi Salama kwa Watoto wa Kike, litafanyika tarehe 2 Agosti 2026, katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro. Kwa mujibu wa Waratibu wa kampeni hiyo kutoka The Brighter Binti Foundation, Dkt. Kyobya anatarajiwa kuzindua daraja la Utalii katika njia ya Sonjo Route tayari kwa matembezi ya vilimani. "Agosti 2, saa 1:00 Asubuhi, Mkuu wa Wilaya Dkt. Kyobya atazindua rasmi daraja la Utalii, kisha kufanya 'Hike' njia ya maporomoko ya maji ya Sanje ambapo washiriki wote tutajumuika," wamesema waratibu hao. Mchana, matukio mengine yatafanyika Shule ya Sekondari Sanje ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo: Mawasilisho mafupi ju...

SERIKALI NA WAWEKEZAJI & WATOA HUDUMA MIGODINI WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO KWENYE SEKTA YA MADINI*

▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji ▪️ Wadau wapongeza hatua za serikali za kutatua changamoto ▪️Waziri Mavunde awataka Watanzania kuanza ujenzi wa viwanda vya bidhaa za migodini ▪️ Kampuni ya MANTRA yanuia kuiweka Tanzania kwenye kumi bora ya wazalishaji wa Uranium Duniani Dar es salaam Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya madini kupitia majukwaa ya majadiliano kwa lengo la kujenga sekta yenye ushindani, inayovutia uwekezaji na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Mhe. Mavunde ameyasema hayo katika kikao cha Mining Breakfast Briefing (*MBB*), kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa Chemba ya Migodi Tanzania(TCM) na Wizara ya Madini, ambapo ametoa wito kwa wadau kuendelea kutumia majukwaa hayo kujadili fursa na changamoto zinazohusu sekta ya madini. Amewashukuru viongozi na wanachama wa Chemba ya Migodi Tanzania kwa kuendelea kutoa nafasi ya Serikali na wadau kukutana na kujadiliana kuhus...