Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga imeendelea kuwaomba wafanyabiashara kulipa kodi Kwa hiyari na Kwa wakati ili kujiepusha na adhabu zitokanazo na kuchelewa kulipa Kodi ikiwemo faini.
Rai hiyo imetolewa na meneja wa TRA mkoa Castro John alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari ofisini kwake kufuatia ongezeko la makusanyo ya Kodi tangu walipoadhimisha miaka 30 ya kuanzishwa Kwa mamlaka hiyo ambapo ndani ya miezi miwili wameweza kukusanya kiasi zaidi ya lengo.
"TRA mwaka huu tumesherehekea miaka 30 niwashukuru sana walipa Kodi wa mkoa wa Tanga muitikio umekuwa mkubwa kwenye miezi miwili kutoka mwezi July hadi August 2026 tume fanya vizuri tulipangiwa kukusanywa shilingi Billion 75.7 lakini tumevuka lengo na kukusanya Billion 104.9 sawa na asilimia 139"
Castro pia amevipongeza vyama vya wafanyabiashara kama Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT),TNCC,TWCC wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuhakikisha TRA wanafanya vizuri na makusanyo ya serikali yanakusanywa.
Pia amewataka wafanyabiashara kutumia mipaka rasmi kwani endapo atabainika na kukamatwa kulingana na Sheria zilizopo kwa upande wa forodha mzigo wote unaweza kutaifishwa,chombo kilichobeba mizigo pia kuchukuliwa na hata mfanyabiashara wenyewe kuweza kuishia gerezani.
Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara pamoja na wananchi Kwa ujumla kuzingatia takwa la kiserikali la kudai na kutoa risiti pale wanapofanya huduma au manunuzi.

Comments
Post a Comment