Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Wamiliki wa gereji zenye vibali vya kutengeneza magari ya serikali mkoani Tanga wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kupokea magari hayo ya serikali na kuyafanyia Matengenezo bila kuwa na kibali Cha gari husika kutoka TEMESA.
Agizo hilo limetolewa na meneja wa TEMESA mkoa wa Tanga Mhandisi Jamal Waziri kufuatia baadhi ya wamiliki wa gereji kufanya kazi kinyume na taratibu zilizopo.
Aidha Mhandisi Jamal ameainisha gereji hizo kuwa ni LAL GROUP OF CAMPANY, TOYOTA, na ADAMS MOTOR na kusema kuwa hizo ndizo zenye vibali/ithibati ya kutengeneza magari ya serikali kwa mkoa wa Tanga lakini hawapaswi kutengeneza mpaka kuwa na kibali cha gari husika.
"Yaani kuwa na kibali kutoka TEMESA haimaanishi kwamba wanaruhusiwa kupokea kila gari,isipokuwa ni gari litakalofika kwao liwe na kibali sasa cha matengenezo husika,sasa baadhi yao wamekuwa wakikaidi na kufanya wanavyotaka wao ila hii itawagharimu kwani hata hicho kibali tutamfutia kabisa kwani kufanya matengenezo bila kibali ni kosa kisheria", alisema Jamal.
Jamal pia ametoa angalizo juu ya vibali vinavyotolwa Kwa sasa kuwa sio vya makaratasi tena bali kila kitu ni mfumo hivyo wanapaswa kuwa makini zaidi.
Kwa Upande meneja wa kampuni ya TOYOTA Vimal Upadhyay hapa Tanga ameiomba TEMESA kuwa na utaratibu wa kuwapatia kazi kwa usawa kwani wanatumia gharama kubwa kulipia vibali lakini wanajikuta hawnufaiki na zaidi ni kupata hasara.
" Tunajitahidi kulipia kibala kwa wakati ambapo tunatoa pesa nyingi lakini kazi hatupati kutoka TEMESA sasa tunashindwa kuelewa kwanini wakati kama ni vifaa hapa TOYOTA hakuna kifaa ambacho hatuna na mafundi wenye uwezo mkubwa tunazo,tunawaomba watuangalie kwa jicho la tatu ", alisema Upadhyay.
Upadhyay pia aliongeza kuwa kuna magari mengi ya serikali aina ya TOYOTA hivyo ni vema wakawa wanapatiwa wao wenyewe kuyafanyia matengenezo kwani vifaa wanavyo.

Comments
Post a Comment