Kutokana na baadhi ya wafanyabiashara nchini kutumia vipimo visivyo sahihi katika kuwahudumia wananchi, Wakala wa Vipimo Nchini (WMA) umewaonya wafanyabiashara wanaotumia vipimo visivyokidhi viwango kuwa wanakabiliwa na adhabu kali kwa mujibu wa sheria, ikiwemo faini na kifungo. Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 18, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, Mtumba jijini Dodoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo nchini (WMA), Alban Kihulla, amesema mtuhumiwa anayekubali kosa anaweza kutozwa faini ya Shilingi 100,000 hadi milioni 20 kwa kosa moja. Amesema kwa anayekataa kosa na kupatikana na hatia mahakamani, adhabu ni faini ya Shilingi 300,000 hadi milioni 50, au faini pamoja na kifungo kisichozidi miaka miwili. Kwa mkosaji wa mara kwa mara, amesema faini inaweza kufikia Shilingi milioni 100 kwa kosa moja, hatua inayolenga kuhakikisha wafanyabiashara wanatumia vipimo sahihi na kulinda haki za walaji. Kihulla amewataka wafanyabiashara na wakulima kuachana ...
Marato tv - Sauti ya Jamii