Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

OCPD INAVYOWEKA MSINGI WA KISHERIA WA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050

Maendeleo ya Taifa hayaishii kwenye kuwa na sera nzuri, mipango mikubwa au dira yenye malengo makubwa lakini nyuma ya kila hatua ya maendeleo inayokusudiwa kutekelezwa, kuna msingi mmoja muhimu unaowezesha Serikali kuchukua hatua kwa uhalali, utaratibu na uwajibikaji.

Dira inaweza kuonyesha Tanzania inayotakiwa kujengwa, sera inaweza kuelekeza namna ya kufikia malengo hayo na mipango ikaainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Hata hivyo, bila mfumo madhubuti wa sheria unaoenda na wakati malengo hayo yanaweza kubaki kwenye nyaraka badala ya kugeuka kuwa matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi.

Hapa ndipo nafasi ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) inapofanya kazi kubwa katika kufikia lengo hilo la serikali na jamii kwa ujumla. Kupitia maandalizi na uboreshaji wa sheria Ofisi hii inashiriki katika kuweka msingi wa kisheria unaosaidia Serikali kutekeleza sera, mipango na mikakati yake katika mazingira yanayobadilika kiuchumi, kijamii na kiteknolojia. 

Wajibu wa OCPD katika mchakato huu ni kutafsiri na kuandika katika lugha ya kisheria maono na matakwa ya kisera ili yaweze kutekelezeka. 

Akizungumzia sheria na mabadiliko hayo Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole amesema kama sehemu ya kuendelea kuimarisha mfumo wa sheria ili kuendana na mweleke wa kisera wan chi, katika kipindi cha Januari hadi Julai 2026, OCPD kwa kushirikiana na Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali, iliandaa miswada ya sheria saba (7) iliyolenga kutunga sheria mpya pamoja na kufanya maboresho katika sheria zilizopo.


Miswada hiyo iligusa maeneo mbalimbali yenye umuhimu katika ustawi wa Taifa ikiwemo kupanua wigo wa upatikanaji wa mikopo, biashara na uwekezaji, kilimo, kodi, ardhi, maliasili, usafiri wa anga, haki jinai, Serikali za Mitaa na matumizi ya fedha za umma. Miswada yote ilipitishwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliomalizika tarehe 4 Septemba 2026.

Amesema miongoni mwa Sheria hizo ni Sheria ya Mikopo kwa Dhamana za Mali Zinazohamishika ya mwaka 2026 ambayo inaweka mfumo wa kisheria unaoruhusu mali zinazohamishika kutumika kama dhamana ya mikopo na kuanzisha Masijala ya kusajili maslahi katika mali hizo.

“Hatua hii ni muhimu katika kupanua fursa za kifedha kwa watu na biashara ambazo huenda hazina mali zisizohamishika zinazokubalika kwa urahisi kama dhamana, kwahiyo kutambua mali zinazohamishika kunaweza kupanua wigo wa mali zinazoweza kutumika kupata mitaji, na hivyo kuwezesha biashara kuongeza wigo wa shughuli, uzalishaji, uwekezaji na fursa za ajira” alieleza Bw. Njole.

Aliongeza “Katika mazingira ambayo biashara na uchumi vinaendelea kubadilika, sheria nazo haziwezi kubaki palepale, hivyo kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2026, Bunge ilimefanya maboresho katika sheria 18, huku baadhi yakilenga kuongeza uwazi katika shughuli za biashara na kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu wa kifedha”.

Aidha Mwandishi Mkuuu wa Sheria amesema marekebisho mengine yaliyofanyika ni katika Sheria ya Majina ya Biashara na Sheria ya Kampuni Sura ya 212. 

Mabadilikoa katika sheria hii yanahusu upatikanaji na utoaji wa taarifa kuhusu umiliki manufaa. Kwa mujibu wa marekebisho haya,sasa kampuni za kigeni zinatakiwa kuwasilisha taarifa za wanahisa na umiliki manufaa kama ilivyo kwa kampuni za ndani. 

Bwana Njole amesema hatua hizo zinalenga kuongeza uwazi wa umiliki wa biashara na kuimarisha mapambano dhidi ya utakatishaji fedha, ufadhili wa ugaidi na shughuli nyingine haramu.

“Maboresho hayo yamegusa pia sekta ya usafiri wa anga ambako mfumo wa uchunguzi wa ajali na matukio hatarishi ya ndege umeboreshwa ili kutambua kisheria Kitengo cha Uchunguzi wa Ajali za Ndege, masharti kuhusu uhuru wa uchunguzi, ulinzi wa taarifa nyeti na mgongano wa maslahi yanalenga kuimarisha usalama wa usafiri wa anga na kuoanisha mfumo wa Tanzania na viwango vya kimataifa” alifafanua Njole.

Katika mfumo wa haki jinai, Mwandishi Mkuu wa Sheria amesema Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya JinaiSura ya 20 imefanyiwa marekebisho ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuchelewesha kuanzishwa kwa taratibu za jinai pale ambapo jambo lina sura ya madai au kiutawala katika masuala ya ajira. Lengo ni kuhakikisha makosa ya jinai yanashughulikiwa kwa wakati na kwamba haki haicheleweshwi.

Bwana Njole alieleza zaidi, katika kuimarisha urekebishaji na urejeshwaji wa wafungwa katika jamii, Sheria ya Jeshi la Magereza ili kutambua elimu, mafunzo ya ufundi, huduma za kiroho na msaada mwingine kama sehemu ya kuwasaidia wafungwa wanaomaliza vifungo kurejea katika jamii. 

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uandishi wa Sheria kutoka OCPD Bi. Chresencia Mathayo amesema kwa upande wa sekta ya kilimo ambayo ina nafasi muhimu katika maendeleo ya Tanzania, sheria zimepewa mwelekeo wa kusaidia kuongeza tija, ufanisi wa taasisi na ushindani wa mazao.

Amesema Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kilimo ya Mwaka 2026 imefanya marekebisho katika sheria zinazohusu usalama wa chakula, mkonge, sukari na chai.

“Mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha mamlaka za udhibiti, kuboresha utatuzi wa migogoro baina ya wakulima na wafanyabiashara na kupunguza muingiliano wa majukumu ya taasisi, na katika mwelekeo huo, Wakala wa Maendeleo ya Chai umefutwa na majukumu yake sasa yanatekelezwa na Bodi ya Chai hatua inayolenga kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali na kuongeza ufanisi” Alieleza Bi. Mathayo.

Aidha ameongeza kuwa hatua nyingine imechukuliwa ni kufuta Sheria ya Kufuta Sheria ya Tasnia ya Pareto Sura ya 376 na majukumu ya Bodi ya Pareto yaliyokuwa yameanzishwa chini ya Sheria hiyo na kuhamishiwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) sambamba na mali, madeni na watumishi wa Bodi huyo. 

Lengo ni kupunguza uwepo wa taasisi zinazotekeleza shughuli zinazofanana, kuimarisha uratibu na kuongeza tija katika matumizi ya rasilimali za umma.

Ameongeza kuwa mabadiliko katika mfumo wa sheria yamegusa pia ardhi, maliasili na mazingira ya uwekezaji ambapo Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi imefanyiwa marekebisho ili kuimarisha ushirikiano kati ya Tume na mamlaka nyingine za upangaji wa matumizi ya ardhi na kupunguza mwingiliano wa majukumu. Adhabu nazo zimeboreshwa ili kuendana na mazingira ya sasa na kuongeza uzingatiaji wa sheria.

Mkurugenzi huyo ameeleza katika eneo la rasilimali asilia, marekebisho yamekusudia kuweka mazingira bora ya uwekezaji kwa kupanua wigo wa maeneo ambako mashauri yanayohusu migogoro ya uziduaji, uvunaji, upatikanaji au matumizi ya mali na rasilimali asilia yanaweza kusikilizwa kwa kuzingatia makubaliano ya wahusika.

Akizungumzia mabadiliko katika utawala wa Serikali za Mitaa Bi. Mathayo amesema marekebisho yameelekezwa katika kuoanisha muda wa madaraka ya viongozi wasaidizi, wakiwemo Makamu Wenyeviti na Naibu Meya, na muda wa viongozi wakuu husika, hatua inayolenga kuimarisha uwajibikaji na mwendelezo wa uongozi.

Kwa upande wa uhifadhi Wanyamapori, Bi. Mathayo amefafanua kuwa marekebisho yanapendekeza kuondoa mifugo miongoni mwa mali zinazoweza kutaifishwa baada ya mtu kutiwa hatiani kwa kosa chini ya sheria hiyo.

“Sheria ya Uthamini nayo imefanyiwa marekebisho ili kuongeza uwazi, kuweka matumizi sahihi ya misingi ya uthamini na kuhakikisha shughuli za kitaalamu zinafanywa na watu waliosajiliwa au kutambuliwa kwa mujibu wa sheria” Alieleza Bi. Mathayo. 

Aliongeza “Katika upande wa uchumi na utekelezaji wa bajeti, Sheria ya Fedha ya mwaka 2026 imefanya marekebisho katika sheria 26 za kodi na zisizo za kodi, mabadiliko hayo yanahusu baadhi ya kodi, tozo na ada, pamoja na hatua za kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato na kuboresha mazingira ya biashara”.

Mkurugenzi huyo wa Uandishi wa Sheria amesema marekebisho hayo yanalenga pia kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta za kimkakati zikiwemo viwanda, kilimo, nishati na afya.

“Maboresho haya yanatoa ujumbe mpana zaidi kuhusu nafasi ya sheria katika maendeleo ya Taifa. Sheria bora inapaswa kutoa uhakika, kulinda haki, kuweka uwajibikaji, kuondoa vikwazo visivyo vya lazima na kufungua fursa za maendeleo. Hivyo basi, miswada iliyoshughulikiwa katika kipindi cha Januari hadi Julai 2026 ni zaidi ya marekebisho ya vifungu vya sheria. 

Ni sehemu ya safari ya kujenga mfumo wa sheria unaoendana na mahitaji ya Tanzania ya sasa na unaoweka msingi wa Tanzania inayokusudiwa kujengwa katika miongo ijayo”. alibainisha Bi. Chresencia.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...