RC SAGINI AJITAMBULISHA RASMI CCM MBEYA, AWEKA MSISITIZO UTEKELEZAJI WA ILANI NA USHIRIKIANO KATIKA KUHARAKISHA MAENDELEO
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Jumanne Abdallah Sagini, amefanya ziara rasmi katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya zilizopo jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha rasmi kwa viongozi wa chama pamoja na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya Mkoa.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Septemba 18, 2026, Mhe. Sagini amekutana na viongozi wa CCM Mkoa wa Mbeya, ambapo ameeleza umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na chama katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Amesisitiza kuwa Serikali ya Mkoa wa Mbeya itaendelea kuhakikisha ahadi na maelekezo yaliyopo katika Ilani ya Uchaguzi yanatekelezwa kwa vitendo, huku maslahi na mahitaji ya wananchi yakiendelea kuwa sehemu ya msingi katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.




























Comments
Post a Comment