Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS SAMIA AZINDUA TUME MAALUMU KUBAINI CHANZO NA WAHUSIKA WA GHASIA ZA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI 2025

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua Tume ya Rais ya Uchunguzi ya Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria Katika Matukio ya Ghasia Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ikiwa na jukumu la kuchunguza kwa kina chanzo cha matukio hayo, wahusika pamoja na waliowezesha kutokea kwake. Akizungumza leo Ijumaa Agosti 7, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Tume hiyo, Rais Samia amesema ameunda Tume hiyo kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Tume ya Uchunguzi, Sura ya 32, ili kuwezesha uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya ghasia na ukiukwaji wa sheria yaliyotokea. Amesema Tume hiyo itaongozwa na Jaji Shabani Ally Lila na itakuwa na jumla ya makamishna sita, ambapo mmoja anatoka Uganda na mwingine Namibia, hatua inayolenga kuongeza mtazamo mpana katika utekelezaji wa jukumu hilo. “Katika Tume hii tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka nje ya Tanzania ili kupata maono mapana,” amesema Rais Samia. Rais Sami...

TUMIENI MUDA VIZURI MNAPOPATA NAFASI YA KWENDA JKT- MHE PINDA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo  Pinda, amewataka Vijana nchini kutumia muda vizuri wanapopata nafasi ya kwenda Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT). "Sisi tuliopita JKT miaka ya zamani huko, hatuna budi kuwaambia vijana wa leo kwamba tumieni muda  huu vizuri mnapopata nafasi ya kwenda JKT, JKT ambayo sasa inalenga kuwaimarisha vijana na kuwapa uwezo wa kuweza  kuanza maisha yao wenyewe kutokana na ujuzi walioupata kutoka maeneo ya makambi ya JKT" Mhe. Pinda ameyasema hayo Agosti 6,2026 wakati alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane), yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni Dodoma. Amefafanua kuwa JKT ni shule nzuri kwa vijana, kwani limetengeneza utaratibu mzuri wa kuwapa mafunzo vijana hususani katika suala zima la ubunifu. Vijana wanafundishwa ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

SAUTI YA SERENGETI YANG'ARA KATIKA JUKWAA LA KIMATAIFA RWANDA

 SAUTI ya Jimbo la Serengeti imeendelea kusikika katika majukwaa ya kimataifa baada ya kushiriki katika programu ya African Leadership for Women in Political Leadership (AWPL) inayowakutanisha viongozi wanawake kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika kwa lengo la kuimarisha uwezo wa uongozi, kubadilishana uzoefu na kujenga mtandao wa viongozi wanawake wenye ushawishi katika maendeleo ya bara. Katika mjadala huo, swali lilielekezwa kwa Bi. Ahunna Eziakonwa, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika, likitaka kufahamu nafasi ya AWPL katika kuwawezesha wanawake wanaoshika nafasi za juu za uongozi, ikiwemo urais, kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuongozi, misukosuko ya kisiasa pamoja na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yanayoendelea kushuhudiwa katika nchi za Afrika. Swali hilo pia lilitaka kuelewa kwa undani namna ambavyo programu hiyo inaendelea kuwapa viongozi wanawake ushauri, mafunzo na mifumo ya usaidizi inayowawezesha kufanya maamuzi yenye tija, ku...

CENTRAL BANK LIFTS RESTRICTIONS AS TANZANIA OPENS TREASURY MARKET TO GLOBAL INVESTORS

 By Prosper Makene  The Bank of Tanzania has announced new amendments that now allow all non-resident investors to participate in the government securities market, including Treasury bills and bonds issued by the United Republic of Tanzania. The notice was signed by Bank of Tanzania Governor Emmanuel M. Tutuba. In a public notice issued on 6th August 2026, the Central Bank said the Foreign Exchange (Amendment) Regulations, 2026 were published in Government Gazette Notice No. 206 of 2026 on 17 July 2026 under the Foreign Exchange Act, Cap. 271. According to the Bank, the reform is aimed at broadening access to the domestic financial markets and strengthening Tanzania’s position as an attractive investment destination. Prior to the amendment, participation in the government securities market was restricted to residents of the East African Community (EAC), the Southern African Development Community (SADC), and members of the Tanzanian diaspora community. “The amendments, among ot...

TANZANIA: MAREKEBISHO MAPYA YARUHUSU WAGENI KUWEKEZA KWENYE DHAMANA ZA SERIKALI-BOT

 Na Mwandishi Wetu  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza mabadiliko makubwa katika sheria za uwekezaji. Kwa mara ya kwanza, sasa watu wote wanaoishi nje ya nchi wanaruhusiwa kuwekeza kwenye dhamana za Serikali. Hii inajumuisha Hazina za muda mfupi na Bondi za muda mrefu zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Taarifa ambayo imetolewa rasmi na Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel M. Tutuba, tarehe 6 Agosti 2026 imesema kuwa Benki Kuu imefanya mabadiliko hayo kupitia Kanuni mpya za Fedha za Kigeni (Marekebisho) za Mwaka 2026. Kanuni hizo zilichapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 206 tarehe 17 Julai 2026, chini ya Sheria ya Fedha za Kigeni, Sura ya 271. Kwa miaka mingi, ni makundi machache tu yaliyokuwa yakiruhusiwa kuwekeza. Haya yalijumuisha wakazi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, pamoja na Watanzania walioko nje ya nchi. Lakini sasa mlango umefunguliwa kwa kila mtu. Kwa mujibu wa Benki Kuu, mwek...

CHANDE AVUTIWA NA HUDUMA ZA TADB NANENANE

 NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, amesema Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inaendelea kuwa chachu ya mageuzi katika sekta ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima, wafugaji na wadau wa mnyororo wa thamani kupata huduma za kifedha zinazoongeza uzalishaji na tija. Mhe. Chande ameyasema hayo alipotembelea banda la TADB katika Maonesho ya 32 ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea jijini Dodoma, ambapo alijionea huduma na programu mbalimbali zinazotekelezwa na benki hiyo kwa lengo la kukuza kilimo chenye tija na biashara. Baada ya kupokea maelezo kutoka kwa wataalamu wa TADB, Naibu Waziri ameeleza kuridhishwa na namna benki hiyo inavyotekeleza dhamira yake ya kuwafikia wadau wa sekta ya kilimo kupitia mikopo na huduma nyingine za kifedha zinazowawezesha kuongeza uzalishaji, thamani ya mazao na kipato. Amesema hatua hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa yenye tija, inaimarisha usalama wa chakula, inafungua fursa za ajira n...