HALMASHAURI 39 ZAANZA KUHOJIWA NA LAAC KWA HOJA ZA CAG MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mhe. Ado Shaibu Ado, amesema kamati hiyo imeanza zoezi la kuwahoji viongozi wa 39 kutoka mikoa 15 nchini kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Akizungumza na waandishi wa habari leo Bungeni Jijini Dodoma Ado amesema zoezi hilo linafanyika kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likiwa na lengo la kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma katika mamlaka za serikali za mitaa. "Kamati ya LAAC inapata nafasi ya kuwahoji wakurugenzi wa halmashauri pamoja na menejimenti zao kuhusu masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na CAG, lakini pia tunafuatilia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na kamati katika vikao vya awali na yale yaliyotolewa na CAG," amesema. Ameeleza kuwa Spika wa Bunge alitoa kibali kwa kamati hiyo kuendelea na zoezi hilo baada ya hatua ya awali iliyofanyika wakati wa Bunge...
Marato tv - Sauti ya Jamii