Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

KAMATI YA LAAC YAANZA KUWAHOJI HALMASHAURI 39 KUTOKANA NA RIPOTI YA CAG

 HALMASHAURI 39 ZAANZA KUHOJIWA NA LAAC KWA HOJA ZA CAG MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mhe. Ado Shaibu Ado, amesema kamati hiyo imeanza zoezi la kuwahoji viongozi wa 39 kutoka mikoa 15 nchini kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Akizungumza na waandishi wa habari leo Bungeni Jijini Dodoma Ado amesema zoezi hilo linafanyika kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likiwa na lengo la kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma katika mamlaka za serikali za mitaa. "Kamati ya LAAC inapata nafasi ya kuwahoji wakurugenzi wa halmashauri pamoja na menejimenti zao kuhusu masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na CAG, lakini pia tunafuatilia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na kamati katika vikao vya awali na yale yaliyotolewa na CAG," amesema. Ameeleza kuwa Spika wa Bunge alitoa kibali kwa kamati hiyo kuendelea na zoezi hilo baada ya hatua ya awali iliyofanyika wakati wa Bunge...

VIJANA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA ZA MADINI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 📍DODOMA Vijana nchini wamehimizwa kutumia nguvu kazi, maarifa na ubunifu wao kuchangamkia fursa zinazotolewa na Sekta ya Madini badala ya kusubiri misaada au mitaji kutoka serikalini, huku wakitakiwa kuanza na rasilimali walizonazo ili kujenga mafanikio ya kiuchumi. Wito huo umetolewa  kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Kitaifa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Xinda Energy Resources Technology Import and Export Trade Co. Ltd, Abia Mafie, aliyesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupitia mafunzo, warsha na programu mbalimbali za uwezeshaji, lakini baadhi yao hushindwa kutumia maarifa hayo kwa vitendo. “Vijana tusisubiri Serikali itupatie kila kitu. Unaweza kuanza na kidogo ulichonacho na ukakua hatua kwa hatua. Watu wengi waliofanikiwa walianza hivyo,” amesema Mafie. Amesema Sekta ya Madini ni miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa za ajira, ujasiriamali na uwekezaji, hususan katika uchakataji na uongezaji thamani wa madini, hatua inayochochea uku...

CHEGE AANDIKA HISTORIA RORYA KWA MPANGO WA UJENZI WA OFISI ZA CCM KUANZIA KATA HADI MATAW

 MBUNGE wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Wambura Chege (JW-Chege), ametangaza mpango mkubwa wa kujenga na kukarabati ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata zote zenye uhitaji ndani ya jimbo hilo, hatua inayotajwa kuwa itaimarisha utendaji wa chama na kuboresha mazingira ya kazi kwa viongozi na watendaji wake.  Mpango huo umetangazwa wakati wa kikao cha Halmashauri ya CCM Wilaya ya Rorya, ambapo Mhe. Chege alisema dhamira yake ni kuhakikisha chama kinakuwa na miundombinu bora kuanzia ngazi ya wilaya, kata hadi matawi, ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wanachama na wananchi. Katika kuonyesha utekelezaji wa ahadi hiyo, Mbunge huyo ametoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi mpya ya CCM Wilaya ya Rorya, huku akieleza kuwa watendaji wa chama wanatarajiwa kuhamia katika jengo hilo ndani ya mwezi Agosti mwaka huu. Mbali na kukamilisha jengo la ofisi za wilaya, Mhe. Chege ameagiza kufanyika kwa upimaji wa eneo na uch...

WAZIRI KIJAJI: NANENANE NI JUKWAA MUHIMU KUKUZA UTALII WA NDANI

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane 2026 ni jukwaa muhimu la kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii barani Afrika, huku yakitoa fursa ya kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maliasili na kuhamasisha utalii wa ndani. Akizungumza leo baada ya kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Dkt. Kijaji amesema wizara imeandaa huduma na maonesho mbalimbali yanayowapa wananchi, hususan wanafunzi, nafasi ya kujifunza kuhusu rasilimali za taifa na kushuhudia baadhi ya wanyamapori hai ili kuongeza uelewa kuhusu urithi wa asili wa Tanzania. "Tupo hapa kwenye Maonesho ya Nanenane tukiwa tumewaletea wananchi huduma mbalimbali. Tunatoa elimu kuhusu uhifadhi na ustawi wa maliasili, lakini pia tumewaleta baadhi ya wanyamapori hai ili wananchi na wanafunzi wapate fursa ya kuwaona na kujifunza kuhusu utajiri mkubwa ambao Mwenyezi Mungu ameijalia Tanzania," ame...

WAKALA WA VIPIMO WAELEZA TIBA YA GESI PUNGUFU

 *Na.WMA-DODOMA*  WANANCHI  wametakiwa kuhakikisha wanapima mitungi ya gesi kabla ya kuinunua ili kujiridhisha kuwa wanapata kipimo cha gesi kinacholingana na fedha wanazolipa, huku wafanyabiashara wote wa gesi wakikumbushwa kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo (WMA). Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Singida, Willie Amosi, wakati wa Maonesho ya 49 ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma ambapo amesema matumizi ya gesi ya kupikia yameongezeka kwa kasi kufuatia jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Amesema jukumu la Wakala wa Vipimo ni kuhakikisha kila mtungi wa gesi unaouzwa kwa wananchi unakuwa na kipimo sahihi cha gesi kama kilivyoainishwa na mzalishaji, ili kumlinda mlaji dhidi ya hasara inayoweza kusababishwa na vipimo visivyo sahihi. "Wananchi wana haki ya kujiridhisha kuwa gesi wanayonunua ina uzito sahihi....

CP MKAMA AIPONGEZA MWANZA KWA USHIRIKIANO WA USALAMA

 Na: Dawati la Habari, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza. Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama , leo Agosti 4, 2026, ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa , aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa. Akimkaribisha, Mkalipa amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuwa salama na wenye utulivu, hali inayowawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kijamii na kiuchumi bila hofu. Amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano imara kati ya Jeshi la Polisi, vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi. Aidha, amemhakikishia CP Mkama kuwa Mkoa wa Mwanza uko tayari kuendelea kupokea ushauri, maelekezo na miongozo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ili kuimarisha utekelezaji wa falsafa ya Polisi Jamii na kudumisha amani na usalama. Kwa upande wake, CP Mkama amesema ziara yake inalenga kutathmini utekelezaji wa shughuli za Polisi Jamii mkoani Mwanza, kupitia mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo na maeneo yanayohitaji...