Jiji la Mwanza limepiga hatua nyingine katika jitihada za kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji baada ya kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi bilioni 39 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Chanzo cha Maji Butimba. Mkataba huo uliosainiwa jijini Mwanza baina ya Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), ni sehemu ya uwekezaji mkubwa unaolenga kuongeza uzalishaji wa maji, kuimarisha miundombinu ya usambazaji na kuhakikisha wakazi wa Jiji la Mwanza wanapata huduma ya maji yenye uhakika. Kwa sasa, Jiji la Mwanza linategemea vyanzo viwili vikuu vya maji vya Butimba na Capri Point ambavyo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha takribani lita za ujazo milioni 138 za maji kwa siku. Hata hivyo, mahitaji ya maji kwa wakazi wa jiji hilo yamefikia takribani lita za ujazo milioni 188 kwa siku, hali inayosababisha kuwepo kwa nakisi ya takribani lita za ujazo milioni 50 za maji kila siku. Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mr...
Marato tv - Sauti ya Jamii