Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MKOPO WA BILLIONI 600 KUTOKA UMOJA WA ULAYA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI SAFI MWANZA

Jiji la Mwanza limepiga hatua nyingine katika jitihada za kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji baada ya kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi bilioni 39 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Chanzo cha Maji Butimba.

Mkataba huo uliosainiwa jijini Mwanza baina ya Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), ni sehemu ya uwekezaji mkubwa unaolenga kuongeza uzalishaji wa maji, kuimarisha miundombinu ya usambazaji na kuhakikisha wakazi wa Jiji la Mwanza wanapata huduma ya maji yenye uhakika.


Kwa sasa, Jiji la Mwanza linategemea vyanzo viwili vikuu vya maji vya Butimba na Capri Point ambavyo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha takribani lita za ujazo milioni 138 za maji kwa siku.

Hata hivyo, mahitaji ya maji kwa wakazi wa jiji hilo yamefikia takribani lita za ujazo milioni 188 kwa siku, hali inayosababisha kuwepo kwa nakisi ya takribani lita za ujazo milioni 50 za maji kila siku.

Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Chanzo cha Maji Butimba unatarajiwa kuwa suluhisho muhimu katika kupunguza pengo hilo, ambapo baada ya kukamilika utaongeza uwezo wa uzalishaji wa maji hadi kufikia takribani lita za ujazo milioni 170 kwa siku.

Mradi huo ni sehemu ya programu ya LV WATSAN na unatarajiwa kugharimu zaidi ya Shilingi bilioni 600. Katika utekelezaji wake, Serikali ya Tanzania itanufaika na mkopo wa Euro milioni 190 kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) pamoja na washirika wengine wa maendeleo, huku pia ikipata mkopo wenye masharti nafuu wa Euro milioni 12.93 kutoka Umoja wa Ulaya.

Fedha hizo zinalenga kuongeza uwezo wa miundombinu ya maji na usafi wa mazingira, sambamba na kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutokana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Mwanza.

Akizungumza katika hafla ya kusainiwa kwa mkataba huo, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Christine Grau, amesema uwekezaji huo ni sehemu ya ushirikiano wa muda mrefu wa zaidi ya miaka 50 kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.

Amesema kupitia mkakati wa Global Gateway, Umoja wa Ulaya pamoja na nchi wanachama wake wameendelea kuiunga mkono Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya maji, nishati safi, mabadiliko ya kidijitali na maendeleo ya kilimo.

"Mwaka jana tuliadhimisha miaka 50 ya ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania. Leo tunaendelea kujenga ushirikiano huo kupitia uwekezaji katika sekta ya maji na usafi wa mazingira kwa manufaa ya wananchi wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla."

Balozi Grau amesema Mwanza ina nafasi muhimu kiuchumi kutokana na kuwa lango la Jumuiya ya Afrika Mashariki, jambo lililofanya jiji hilo kuwa miongoni mwa maeneo yanayonufaika na ushirikiano kati ya Tanzania na Team Europe.

Amesema Umoja wa Ulaya umeendelea kuona matokeo ya miradi inayofadhiliwa mkoani Mwanza, ikiwemo mradi wa SASA, huku sekta ya maji ikiendelea kuwa eneo la kipaumbele.

Aidha, ameishukuru Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Wizara ya Maji na viongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano waliouonyesha katika maandalizi na utekelezaji wa miradi hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), amesema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya washirika wa maendeleo kuendelea kuunga mkono Tanzania katika kuboresha huduma muhimu kwa wananchi.

"Uwekezaji katika sekta ya maji una mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii na uchumi. Kupatikana kwa maji ya uhakika kunasaidia afya, biashara na maendeleo ya wananchi kwa ujumla."

Naye Meneja wa Programu za Miundombinu kutoka Ofisi ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhandisi Ally Chande, amesema Umoja wa Ulaya umekuwa mshirika wa karibu wa Mwanza katika sekta ya maji kwa zaidi ya miaka 20.

Amesema mbali na utekelezaji wa Butimba Phase Two, Umoja wa Ulaya unaendelea kutathmini uwezekano wa kusaidia maandalizi ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji katika eneo la Kabangaja, kitakacholenga kuongeza upatikanaji wa maji katika maeneo ya kaskazini mwa Jiji la Mwanza.

"Kwa zaidi ya miaka 20 tumekuwa tukishirikiana na Tanzania katika miradi ya maji Mwanza. Tunaendelea kuangalia hatua zinazofuata ili kuhakikisha huduma ya maji inaendana na ukuaji wa jiji."

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Maji, Mhandisi Charles Mwafwili, amesema mradi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kutatua changamoto ya maji katika Mwanza.

"Mradi huu utaongeza uzalishaji wa maji, kupunguza pengo lililopo kati ya mahitaji na uzalishaji wa sasa, na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi."

Awamu ya Pili ya Mradi wa Chanzo cha Maji Butimba inatarajiwa kuanza kutekelezwa katika kipindi kifupi kijacho na kukamilika ndani ya miezi 12 hadi 24.

Kwa wakazi wa Mwanza ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji, mradi huu unatajwa kuwa hatua muhimu kuelekea kuhakikisha huduma ya maji inakwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa jiji hilo.


Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...