Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TVLA YAWATAKA WAFUGAJI KUONGEZA MWITIKIO WA CHANJO ZA MIFUGO


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi, amewataka wafugaji nchini kuongeza mwitikio wa kuchanja mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali ili kuimarisha afya ya mifugo, kuongeza uzalishaji na kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Dkt. Bitanyi ametoa wito huo leo, Juni 18, 2026, mjini Morogoro wakati wa kikao cha pamoja kati ya TVLA na timu ya Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) unaotekelezwa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Kikao hicho kililenga kujadili maeneo ya ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo.


Amesema bado kuna mwitikio mdogo wa wafugaji wadogo katika kuchanja mifugo yao licha ya uwepo wa chanjo zinazozalishwa na TVLA, huku wafugaji wakubwa wakionesha ushiriki mkubwa zaidi katika kampeni za chanjo.

“Tunaona mwitikio mkubwa zaidi miongoni mwa wafugaji wakubwa, lakini kwa wafugaji wadogo bado ni mdogo. Tunao utaalamu na wataalamu. Kupitia mradi huo, elimu kuhusu umuhimu wa chanjo itolewe kwa wafugaji, hususan katika maeneo yenye wafugaji wadogo. Hivyo, tutapunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa ya mifugo,” amesema Dkt. Bitanyi.

Amesema moja ya maeneo yanayopaswa kupewa kipaumbele kupitia C-SDTP ni udhibiti wa ugonjwa wa tupa mimba (Brucellosis), ambao ni miongoni mwa magonjwa yanayoathiri mifugo na kupunguza uzalishaji wa maziwa.

“Kupitia mradi huu tunapaswa kushirikiana kwa pamoja kutokomeza magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, hasa yale yanayopatikana katika mnyororo wa thamani wa maziwa. Ni muhimu pia wananchi wakapatiwa elimu kuhusu dalili za magonjwa hayo ili waweze kupata matibabu kwa wakati na kuepuka maambukizi,” amesema.

Aidha, aliwasisitiza wananchi kutumia maziwa salama na kuhakikisha wanachemsha maziwa kabla ya kuyatumia ili kujikinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kupitia maziwa yasiyo salama.

Dkt. Bitanyi amesema TVLA ina jukumu la kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, kuzalisha chanjo, kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi, kudhibiti ubora wa viuatilifu vya mifugo pamoja na kupima ubora na usalama wa vyakula vya mifugo.

Amesema TVLA pia inaendelea kuimarisha afya ya mifugo kupitia uzalishaji wa chanjo, tafiti na utoaji wa ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji ili kuongeza tija katika sekta ya mifugo.

“TVLA imejikita katika kuhakikisha mifugo inalishwa vyakula vyenye ubora na virutubisho sahihi ili kuongeza afya na tija ya uzalishaji. Sambamba na hilo, tunaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji nchini ili kuboresha mifumo ya ufugaji na kudhibiti magonjwa kwa wakati,” amesema.

Ameongeza kuwa TVLA huzalisha aina saba za chanjo za mifugo zinazotumika nchini, ambapo chanjo moja ni ya kuku na nyingine ni za wanyama kama ng’ombe, mbuzi na wanyama wengine.

Kwa mujibu wa Dkt. Bitanyi, kulinda afya ya mifugo ni hatua muhimu katika kulinda afya ya binadamu kwa kuwa takwimu za dunia zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya magonjwa yanayowapata binadamu yanatokana na wanyama.

“Ukidhibiti magonjwa kwa mifugo, unakuwa umedhibiti pia magonjwa kwa binadamu. Ndiyo maana afya ya mifugo ni sehemu muhimu ya afya ya jamii kwa ujumla,” amesema.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kitaifa wa C-SDTP, Lazaro Kapela, amesema mradi huo unatekelezwa katika mikoa minane na halmashauri 21 za Tanzania Bara pamoja na mikoa mitano ya Zanzibar.

Amesema mradi huo wa kimkakati unalenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji, zikiwemo upatikanaji wa mbegu bora za ng’ombe kupitia teknolojia ya uhimilishaji, upatikanaji wa malisho bora, huduma za afya ya mifugo pamoja na miundombinu ya maji.

“Bila malisho bora na maji ya kutosha, ng’ombe hawezi kuwa na afya nzuri wala kuzalisha maziwa ya kutosha. Kupitia mradi huu tunafanya uwekezaji katika visima, mabwawa ya maji na mifumo ya kuboresha uzalishaji wa malisho ili kuongeza tija kwa wafugaji,” amesema Kapela.

Ameongeza kuwa mradi huo pia unashirikiana na TVLA katika kuimarisha afya ya mifugo kupitia matumizi ya chanjo na huduma za kitaalamu zinazolenga kuongeza uzalishaji wa maziwa na kupunguza hasara zinazotokana na magonjwa.

Kapela amesema mradi huo utawekeza pia katika vituo vya kukusanyia maziwa ili kuwaunganisha wafugaji na masoko na kuwahakikishia soko la uhakika la mazao yao.

“Vituo vya kukusanyia maziwa vitakuwa kiunganishi muhimu kati ya mfugaji na soko. Lengo ni kuhakikisha mfugaji apate soko la uhakika na thamani stahiki ya bidhaa zake,” amesema.

Amebainisha kuwa mradi huo wa miaka 10 ulianza mwaka 2024 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2034 kwa gharama ya dola za Marekani milioni 231.

Naye Afisa Mwandamizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mradi huo, Goodluck Masawe, amesema mradi unatarajiwa kunufaisha kaya 140,000 sawa na watu zaidi ya 700,000.

Amesema kati ya wanufaika hao, asilimia 40 ni wanawake, asilimia 30 ni vijana na asilimia tatu ni watu wenye ulemavu watakaofikiwa moja kwa moja na huduma za mradi huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Benezeth Lutenga Malinda, amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na wizara hiyo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, ubora na usalama wa mazao ya mifugo kwa masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amesema wizara imeweka msisitizo katika kuimarisha mifumo ya afya ya mifugo, maabara na ufuatiliaji wa magonjwa ili kuhakikisha maziwa na bidhaa nyingine za mifugo zinazozalishwa nchini zinakuwa salama kwa matumizi ya binadamu.

“Mradi huu umejipanga kuimarisha mifumo ya maabara, ufuatiliaji wa afya ya mifugo na kuhakikisha mifugo inayozalishwa na kusambazwa inakidhi viwango vya ubora na usalama. Tunataka kuona maziwa yanayozalishwa nchini yanakuwa na ubora unaotakiwa na yanakuwa salama kwa mlaji,” amesema Dkt. Malinda.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya wizara, taasisi zake na wadau wa sekta ya mifugo wa Tanzania Bara na Zanzibar utakuwa msingi muhimu wa kufanikisha malengo ya mradi huo.

“Tunatarajia mradi huu kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuimarisha usalama wa chakula na kuboresha lishe ya Watanzania pamoja na kuongeza kipato cha wafugaji kupitia mifumo bora ya uzalishaji na masoko,” amesema.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...